KERO Serikali ijenge haraka barabara ya Mbezi Mpiji

KERO Serikali ijenge haraka barabara ya Mbezi Mpiji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Nikiwa mkazi wa Mpiji ninaiomba serikali ijenge barabara ya Mbezi Mpiji kutokana na ubovu wa barabara ya vumbi iliyopo kwakuwa inasababisha uhaba wa magari ya abiria.

Ukitaka kujua ukubwa wa tatizo hili fika kituo cha daladala Mbezi Asubuhi na jioni uone jinsi maelefu ya watu walivyojipanga kusubiria magari.

Nakwakuwa Mpiji ina wakazi wengi sana na inaendelea kukua kwa kasi nashauri ijengwe barabara ya njia sita kwa maana mbili katikati iwe kwaajili ya mwendo kasi na mbili kila upande ni kwa magari ya kawaida.

Bahati nzuri eneo la barabara lilishapimwa na no pana la kutosha.
 
Back
Top Bottom