Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 275
- 795
Nipende kuwasalimu ninyi nyote, habari za muda huu
Tanzania ni kati ya nchi maskini duniani japo ina rasilimali muhimu na nyingi karibia kila mkoa. Je, tatizo linatokea wapi mpaka ongezeko la vijana wasio na ajira kuendelea kuwa kubwa?
Katika uchumi kuna kitu kinajulikana kama "Demand and Supply" kwamba kwa kila uitaji wa kununua kuwe sawa na kiwango cha bidhaa zilizopo sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Hiyo principle ya uchumi ambayo ilishafanyiwa utafiti na kutiki, kimoja kikiwa kikubwa zaidi ya kingine kutakuwa na madhara katika uchumi.
Mfano endapo uitaji wa kununua bidhaa umekuwa mkubwa kuliko bidhaa zilizopo sokoni kwa ajili ya kuuzwa, tegemea kuona bei ya bidhaa hiyo kupanda kwa sababu kila mtu ataitaji bidhaa hiyo ili aipate.
Kwanini kwenye uzi wangu nimesema sekta mbili muhimu? Ni katika kutaka kuzingatia uhalisia wa nadhalia hiyo ya uchumi kinyume na watu wengi ambao wakitoa mapendekezo ya mafanikio ya uchumi hawazingatii nadhalia hiyo na mwisho wa siku ukija kupima maoni yao kiuchumi unakuta yamepwaya kwa sababu wameongelea upande mmoja na kusahau upande mwingine wa hoja yake endepo utapindua meza na kwenda kichume na mawazo yake nini kitatokea!
Kama point ni demand iwe sawa na supply, mwingine anaweza kusema "production should be equal to consumption" kwamba kiwango cha uzalishaji kiwe sawa na kiwango manunuzi.
Kinyume cha hapo kama ni kwenye biashara kama unazalisha kingi lakini unauza vichache elewa hiyo biashara sio rahisi kuendelea kwa sababu utajikuta gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa kuliko kiwango cha mauzo unayokusanya.
Kwa kusema hivyo napendekeza sekta hizi mbili muhimu serikali iongeze uwekazaji wa kutosha kwenye sekta hizo;
1. Kilimo,
2. Michezo na Muziki
Hizo ndo sekta muhimu kuinua uchumi wa taifa na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wengi chini Tanzania. Mfano kwa mwaka 2014, Tanzania ilikadiriwa kuzalisha vijana zaidi ya laki sita tayari kuingia katika soko la ajira wakati soko lenyewe lilikuwa na uwezo wa kuchukua vijana chini ya 100,000. Kumbe kwa kuangalia maelezo hayo hapo juu tunaona namna tatizo la ajira lilivyokuwa kubwa Tanzania mpaka hivi sasa.
Unaweza kuniuliza kwa nini nimechagua sekta hizo mbili tu na kuacha sekta nyingine kama sekta ya Madini, utalii n.k, jibu ni jepesi tu nimefanya utafiti kwa sekta zote na ndio nikabakiwa na sekta hizo mbili kwamba ni mukombozi kwa vijana endapo serikali kwayo itaongeza uwekezaji.
Unapochagua sekta ya uwekezaji lazima uzingatie kitu inajulika kama " Cost Benefit Analysis" ili mwisho wa siku upate sekta ya kuiendeleza ambayo inaleta matokeo makubwa hasa kwa wananchi wako. Ukisema uendeleze sana sekta ya madini au ya utalii au ya kwa mfano, hizo ni sekta Nzuri kuendelezwa ila zisiwe na kipaumbele cha kwanza katika kuendelezwa kwa sababu ni "sekta baguzi" kwamba zinaitaji watu wachache tena wengi wao wawe wasomi. Lakini tunajua namna mfumo wetu wa elimu usivyo rafiki kwamba idadi ya vijana wengi wanafeli na kushindwa kuendelea na masomo ya juu wanabaki mtaani huku idadi ndogo inayopanda kwenda vyuo vikuu wanashindwa kupambana kwa soko la ajira kutoka na elimu duni itolewayo kwenye vyuo vyetu.
ibaya zaidi tumeingia kwenye muungano wa Afrika Mashariki tukaruhusu sera ya "free mobility of labor force" wakati wenzetu wameboresha mfumo wa elimu yao unawaruhusu vijana wao wengi kuongoza kuajiriwa katika umoja huu.
Na kwa kuzingatia hayo ndo maana nikaja na huu utafiti
Michezo na Muziki.
Napenda sana sekta hii, kwa sababu imeinua sana maisha ya vijana wenzetu wengi. hivi ni nani kwake haoni miziki, tamthilia, movie au michezo? Nani asiyependa vitu hivyo? Vijana wanapata utajiri mkubwa kwenye muziki na michezo. Hivi mnaweza kuniambia Diamond Platinum, Alikiba, Rayvany, Harmonize, Mbana Ali Samatta, Idris Sultan, Vicent Kigosi, Saimon Msuva, Marioo, Darasa, Zuchu, Stive Nyerere, John Boco na wengine wengi wana Academic Masters za masomo gani?!! Utashangaa hawana hiyo elimu tukimaanisha kwamba wengi wao wameishia elimu ya kidato cha nne ila kwa ukwasi wao ni mara hata tano ya wasomi wengi wenye degree na masters tuliopo Tanzania.
Shida sio kusoma hadi masters, shida ni gharama mtu anazotumia kusoma hadi level ya degree au masters halafu unakuja kuwa jobless. Kumbe kama akina Harmonize wasio na elimu ya vyeti wametoboa hadi kuwa wasanii wakubwa wanaoeleweka Afrika na duniani, kumbe serikali kama ingekuwa serious katika kuitendea haki sekta ili ikue zaidi ya hapa ilipo na kuacha tabia ya kuwatumia tu wasanii kipindi cha kampeni ya uchaguzi hakika tungeona mapinduzi makubwa sana na maendeo makubwa kwenye uchumi wetu kwa sababu kadiri mtu mmoja anavyotoka kwenye ukosefu wa ajira na kuingia kwenye ajira hasa Muziki au michezo au filamu reflection yake inaenda kuonekana kwenye ukuzi wa uchumi kwa sababu msanii huyo ataajiri na yeye wataalam wake, atanunua magari, atajenga nyumba n.k
Mfano kutoka kwenye ukurusa wa THE AFRICA REPORT.com uliochapisha andiko tarehe 1/8/2014
Kwamba katika mwaka 2011, serikali ya Nigeria chini ya uongozi wa Bwana Goodluck Jonathan waliweza kutoa kiasi cha shs za kitanzania zaidi ya billion 400 kwa ajili ya kusapoti kazi za wasanii hasa waigizaji wa filamu. Baada ya miaka 3 ya uwekezaji huu, taasisi ya filamu Nigeria ijulikanayo kama Nollywood iliweza kuongeza volume ya uzalishaji huku ikiwa ya pili duniani, wakati huo huo ikaongeza mapato kwenye tasnia hadi nafasi ya tatu nyuma ya Bollywood ya India na Hollywood ya Marekani.
Kwa mfano huo nasema pia sekta michezo, muziki na filamu vinaweza kuleta mapinduzi makubwa, narudia tena hili litafanikiwa tu endapo serikali itaunga mkono kwa vitendo ukuaji wa sekta hiyo.
Kipi kifanywe na Serikali ili kukuza sekta hizo;
1. Sekta ya muziki na filamu;

√ Serikali ihakikishe kila wilaya kuna chuo cha Veta, ndani ya chuo hicho ihakikishe kuna kozi ya kujifunza muziki na filamu hapo pia ihakikishe vyombo vya mziki vya kisasa vinakuwepo ndani ya vyuo hivyo.
✓ pia ndani ya vyuo hivyo, serikali ihakikishe kuna MUSIC/ FILM RECORDING STUDIO yenye hadhi ya kutengeneza muziki au filamu nzuri kutokea huko huko mikoani walipo sio mpaka wasafiri kuja Dar ili waweze kurekodi, hii itasaidia kuongea vipaji vya wasanii wengi visifie mikoani.
Twende kwenye michezo serikali ifanye haya kuleta mapinduzi ya Michezo yenye kuleta mafanikio na ajira kwa vijana.✓ Umitashumita na Umiseta viendelee na mwisho wa siku watoto wenye vipaji wapelekwe kwenye chuo cha michezo.
✓ serikali isimamie na ihakikishe kila timu hasa za ligi kuu na za ligi daraja la kwanza zinakuwa na timu za watoto na vijana wawe wamesajiriwa kwenye hizo team ( hiyo iwe lazima takwa la kisheria)
✓ Viwanja vinavyotumika kuchezewa mpira kwa ligi kuu , hasa pitches lazima viwe vya kiwango cha kimataifa. Pitches zitazoruhusiwa ni kama ile ya Azam complex, uwanja wa Mkapa na uhuru. Ni bora timu zote 18 za ligi kuu kucheza kwenye viwanja 5 vyenye hadhi ya kimataifa kuliko kuonesha mechi za ligi kuu kwenye viwanya vibovu kama vya Namungo, Mwadui, karume musoma N.k viwanja hivyo vinashusha sana hadhi ya ligi kuu yetu Tanzania na mwisho wa siku tunakosa uwekazaji mkubwa kutoka nje ya nchi.
2. Sekta ya kilimo.
Katika kuhakikisha kwamba tuna balance uchumi wa taifa ukue pande zote za manunuzi na uzalishaji, nimeona sekta muhimu ambayo serikali ikiwekeza nguvu nyingi italeta manufaa kwa wengi ni sekta ya kilimo.
> Kwanza sekta ya kilimo sio sekta baguzi kama zilivyo sekta nyingine kama za madini na utalii, kwa maana katika sekta ya kulimo mtu yoyote (msomi na asiye msomi) anaweza kuanza shughuli hii na ikamfanikisha hivyo kina suluhisho la kudumu la ajira kwa maana kila siku uitaji wa bidhaa kutoka mashambani ni mkubwa.
> Pili sekta ya kilimo ndio inatoa uhakika wa ukuaji wa uchumi uliosahii kwa maana kwamba mara nyingi mfuko wa kupanda kwa bei sokoni huwa unasababishwa na kupungua kwa bidhaa na mazao kutoka mashambani. Kwa hiyo kuboresha sekta ya kilimo ni kuboresha uimara wa uchumi wa nchi na wananchi hasa vijana.
Nini kifanywe kuinua sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya uchumi kwa vijana na taifa?
1. Vijana sio kwamba hawataki kufanya shughuli za kilimo no, ni kwa sababu hakuna mazingira wezeshi kwa vijana hao kujihusisha na kilimo. Mfano mapori na mashamba yaliyoshikwa na matajiri bila kuendelezwa yanakodishwa kwa bei kubwa ili kuyapata kwa ajili ya kilimo, hivyo kabla hata kijana hajaanza kulima anakatishwa tamaa kuanza shughuli za kilimo kitokana na gharama kuwa kubwa.
✓ Serikali iamue kutambua idadi ya mapori na mashamba yasiyoendelezwa yaliyoshikwa na matajiri wachache, baada ya serikali kutambua mapori na mashamba hayo iyagawe BURE kabisa kwa vijana waliohamasika kufanya shughuli za kilimo. Vijana hao wanaungana kuanzia wa 5 hadi 10 wanaomba shamba hekali 1 nakupewa bure mikoani huko ili waende wakafanye shughuli za kilimo. Embu fikiria kilimo kitakavyo kua kikubwa kwenye mapori mengi yaliyopo katika nchi. *Hifadhi za taifa hazitaguswa.
✓ Katika mapori na mashamba hayo, serikali inawekeza katika upatikanaji wa maji kwa ajili ya kuhakikisha kilimo cha umwagiliziaji ili vijana watakaoenda kujiajiri huko vijijini wasikose maji ya kutosha kwa ajili ya mazao ya
✓ Mwisho serikali ihakikishe inatenga bajeti kubwa katika ununuzi wa matrekta ambayo iatakuwa ikiyakodisha kwa vijana wanaojihusisha na shughuli za kilimo huko mashamban
Kwa kuzingatia sekta hizo mbili tunaweza kukuza uchumi wetu na wa vijana bila kuleta athari katika maendeleo ya pato la taifa
Shukurani
Upvote
4