Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kila mtu ni shahidi wa kinachoendelea katika upandaji wa bidhaa hapa nchini. Vitu vinapanda kila siku, hasa vitu vyeti kabisa kama Mafuta ya Kula, Michele, Sabuni, sukari miongoni mwa vitu vingine.
Sikufurahishwa na Kauli ya Mhe. Rais, mama yetu Samia Kwa kusapoti na kukazia kabisa kuwa Bidhaa lazima zipande na ziendelee kupanda kutokana na kile kinachoendelea Huko Nchi ya Ulaya mashariki.
Sikufurahishwa Kwa sababu, Rais ni mtu Mkubwa ndani ya nchi, kuongea vile ni kushawishi upandaji wa bei Kwa bidhaa hata ambazo huenda zisingekuwa na ulazima wa kupanda. Wafanyabiashara wajanja wasio wazalendo wataichukulia hii kama upenyo wa kuongeza faida katika bidhaa zao Kwa kuongeza BEI hata Kwa bidhaa ambazo zilikuwa Stock.
Serikali ilipaswa ieleze ni namna gani inaenda kukabiliana na kinachoendelea kwenye hiyo vita huko Ulaya Mashariki na kuhakikisha hakitaathiri uchumi wa nchi yetu.
Serikali ingepaswa iwe imajipanga au iwe ilishajipanga Kwa matukio Kama haya yanayotokea ulimwenguni, haiwezekan vita haina hata miezi mitatu ianze kuathiri nchi yetu Kama kweli tupo Sirius.
Vipi iliendelea Kwa mwaka au miaka kadhaa?
Nilitegemea serikali iweke mpango mkakati na programu za kuhamasisha Wakulima wapande mazao yanayotoa Mafuta Kama Alzeti na ufuta Kwa wingi,
Isaidie kushusha bei za viwakilifu, pembejeo n.k. tena ikiwezekana itoe mikopo Vijana walime Alizeti na ufuta ili kukabiliana na changamoto hii ya upandaji wa BEI za Mafuta ya Kula.
Mbona tuliweza kuhamasisha Chanjo ya Corona? Kwa nini serikali isiweze kuhamasisha watu kwenye kilimo?
Serikali wakati mwingine lazima iwe(Kama haina) hifadhi ya kutosha ya Mafuta Kama Dizeli au petrol ambayo yatatumika Kwa Dharura Kama hizi zinazojitokeza. Viundwe visima vya Mafuta vya kuhifadhia malighafi hiyo Kwa wingi kadiri itakavyowezekana.
Haiwezekani watu tunajua kabisa Mafuta ni bidhaa nyeti inayoendesha uchumi wa nchi katika uzalishaji alafu isiundwe Benki ya Mafuta ili kuokoa jahazi nyakati Kama hizi.
Haya Assume hiyo vita iendelee miaka mitatu, assume hizo nchi tunazozitegemea kwenye Mafuta nazo ziingie kwenye machafuko, si nikusema tutakuwa tumekwama?
Serikali Kama hayo yote yameshindikana basi ingepunguza Kodi kwenye sekta za Mafuta Kwa muda ili Kupunguza huo upandaji wa BEI za bidhaa unaosababishwa na athari za vita.
Kusema ukweli usio na suluhisho Bora haina maana yoyote. Huwaga nasema; Ukweli ni mzuri ikiwa Una Suluhu ya namna ya kuukabili. Ukweli usio na Suluhu hauna maana yoyote.
Ni Sawa na Daktari akuambie Una UKIMWI lakini akashindwa kukwambia namna ya kukabiliana na ugonjwa huo. Ukweli usio na Suluhu hauna tofauti na sumu iuayo, ni bora usisemwe kuliko usemwe alafu ulete athari.
Kusema vitu vitapanda bei ni ukweli lakini vipi kuna namna ya kukabiliana na hali hiyo?
Nafikiri nchi yetu inawatu wengi mno, watu milioni 60 hatuwezi kukosa watu wenye akili na mawazo ya kushauri namna ya kuhakikisha bidhaa hazipandi licha ya athari zinazoendelea kusababishwa na hizo vita za Wazungu huko Ulaya.
Ni lazima tuwaonee huruma wananchi masikini ambao kijiko cha Mafuta ya Kula cha Mia sita kwao mi mtihani Mkubwa.
Kuwa kiongozi ni kutatua matatizo ya Msingi ya watu wako.
Ndugu Viongozi wote Kwa nafasi zenu, nawasihi Kwa heshima kubwa, fanyeni mtakavyoweza kuokoa jahazi. Vitu visipande bei, wakati mnahangaika na Jambo Hilo, tafuteni long-term Plan ya kuhakikisha tatizo la Mafuta likitokea ulimwenguni nchini kwetu ichukue miaka walau mitano au kumi kutuathiri.
Nafahamu changamoto ya mambo haya Kwa kiasi. Najua wapo wanufaika na matukio ya namna hii. Najua gharama za kutekeleza mipango hii inaweza kuwa kubwa, lakini hauwezi kuwa kubwa kushinda akili za watu milion 60 WA nchi yetu, hiyo itakuwa ni matusi makubwa ndani ya taifa letu. Yaani watu milioni 60 tushindwe kutatua matatizo yanayotukabili.
Labda itokane na ubinafsi, fitna, kukomoana, hujuma na kuwa Vibaraka vya wageni wasioipenda nchi hii.
Taikon amemaliza. Tuilinde nchi yetu.
Tuipiganie.
Sabato njema!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam