Serikali ya Tanzania haina dini, lakini, baada ya kufuatilia hili Sakata la Lambalamba, nimebaini kuwa Watanzania wana dini zao na wengi sana wanafuata dini zao za kimila!
Chonde chonde, ni hatari sana kukabili masuala ya imani za watu kinguvunguvu bila kuzama kukaa na waumini husika na kuwaelewa na kuwaelimisha polepole bila kuonyesha dharau!
Sisemi kuwa OCS wa Kabwe alikosea kukabiliana na operation ya kimila ya kupambana na wachawi, aka Lambalamba, ila ilitakiwa busara zaidi na upole katika kulitatua hilo tatizo!
Inafikirisha sana!
Wanasiasa wote! Wafanyabiashara wote! Viongozi wa dini na waumini wao! Maofisini, michezoni, safarini n.k zile imani zinazopigwa vita hadharani ndizo zimetamalaki!
Wabongo wengi, japo wana dini zao official, kwa viwango vikubwa sana dini yao ya pili ni hizi za kienyeji!
... mtu akizidiwa ugonjwa au matatizo lazima akawaone JAMAA! 😅