Amani kwenu wana JF na wadau wote wa elimu! Binafsi nikiwa ni mdau mmojawapo wa elimu ninaiomba serikali hususa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi au TAMISEMI kuangalia kwa upeo nzuri nafasi ya Mratibu Elimu Kata ( MEK). Mratibu Elimu Kata ndiye kiongozi anayesimamia elimu katika ngazi ya kata na ni kiungo muhimu kati ya walimu ngazi ya kata na uongozi wa elimu wilaya. Kwa hivi sasa Mratibu Elimu Kata anasimamia elimu katika ngazi zote mbili yaani elimu ya msingi na sekondari. Dosari kubwa ninayoiona katika eneo hili ni kuwa waratibu walio wengi hasa katika halmashauri elimu zao ni ndogo,wengi wao ni walimu wa cheti ( III A au III B/C) jambo linalosababisha washindwe kufanya kazi zao kwa ufanisi. Kwa mfano,kazi mojawapo ya MEK ni kukagua vifaa vya kazi kwa walimu wake eg;maandalio,maazimio na pia kusimamia tendo la ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi. Sasa kama MEK ana elimu ya cheti anawezaje kumkagua au kumsimamia mwalimu mwenye shahada au stashahada? Katika mazingira kama haya Mratibu hawezi kufanya kazi yake/zake kwa ufanisi na atakutana na changamoto nyingi za kiutendaji. Ninawaomba viongozi wa Elimu kuteua walimu/waratibu wenye sifa ili waweze kusimamia elimu kikamilifu kwani walimu hao wenye sifa za kielimu wapo wengi katika maeneo karibu yote katika halmashauri zetu.