Pesanyingi
JF-Expert Member
- Apr 15, 2023
- 1,157
- 1,983
Wasalamu wakuu.
Kuna video naona inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mtu anayejiita baba levo akidhihaki na kuwafedhehesha walimu wetu wa Tanzania.
Maneno aliyozungumza kupitia chombo cha habari achofanyia kazi si maneno mazuri hata kama yana kweli au si kweli kwani hayana utafiti labda kama ana utafiti aliyofanya wa kisomi aitowe ili serikali ifanyie kazi.
Maneno yale ni kejeli na dharau kubwa kwa walimu wetu.
Ikumbukwe kwamba walimu hao ni waajirawa wa serikali na wengine sekta binafsi.
Kuwadhalilisha walimu vile ni sawa na kuwatukana walimu kupitia chombo cha habari kitu ambacho si sawa kumdhalilisha mtu kwa hali yoyote aliyokuwa nayo.
Ili iwe fundisho kwa wanaojiita waandishi wa habari uchwara kama alivyo huyo baba levo, TAMISEMI, WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOGIA, WIZARA YA HABARI, TCRA pamoja na vyama vinavyotetea haki za walimu wampeleke mahakamani baba levo kwa kesi ya kuwadhalilisha walimu na kuwatoa utu.
Kwanini nasisitiza juu ya baba levo kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na chombo anachofanyia kazi, dharau hizi zinaweza leta mtazamo hasi kwa walimu wetu wanaotufundishia watoto wetu na hata kuwavunja moyo kwa kazi ngumu ya kuwasidia watoto wetu mashuleni wanayoifanya.
Masikitikio yangu sijaona chombo chochote hadi muda huu kilichokemea matamshi, dharau, kebehi na udhalilishaji huo kwa walimu wetu.
Wito pia kwa TCRA fatilieni kwa ukaribu hili wimbi la redio zinazoibuka siku hizi hazina watangazaji waliosoma vyuoni bali zinaokota vijana wasiokuwa na taaluma bali waropokaji na kuwafanya ndiyo watangazaji.