Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Habari kutoka chanzo kinachoaminika ndani ya serikali zinaonyesha kwamba serikali ya awamu ya tano imeendeleza dhana ya kutokuwa na huruma kwa wahanga wa matukio ya maafa kama matetemeko na mafuriko, kwa kuwa kwa makusudi kabisa imeamua kutotenga fedha kwa ajili ya mfuko wa maafa nchini. Imesemwa kwamba mfuko huo hauna fedha za kuweza kufanya jambo lolote la maana kwa ajili ya maafa nchini.
Habari znasema kwamba wananchi wanaokumbwa na maafa kama mafuriko yanayoendelea wasitegemee msaada wowote toka serikalini kwa sababu serikali iliamua hata kukitokea maafa ya namna gani wananchi wanapaswa kusimama kwa miguu yao wenyewe, au kusaidiwa na ndugu zao lakini sio serikali. Hili lilionekana kuwa ndio msimamo wa serikali ya awamu ya tano pale wananchi wa Kagera walipokumbwa na maafa ya tetemeko, ambapo Raisi Magufuli aliweka wazi kwamba serikali isingetoa msaada kwa wananchi, na fedha za misaada zingeelekezwa sehemu nyingine sio kuwasaidia wananchi.
IKiwa hili likithibitishwa kuwa kweli, basi ni jambo la kujiuliza ni kwa nini Wabunge hawakuhoji jambo hili Bungeni kwamba kama taifa tunaishi kwa kudura za mwenyezi Mungu bila kuwa na fedha kwa ajili ya mfuko wa maafa! Ikumbukwe kwamba fedha za mfuko wa maafa si kwa ajili tu ya kuwasiaidia wananchi, bali pia kuendesha kampeni za uokoaji na hata kutoa huduma za dharura kwa wahanga wa maafa. Ni ajabu kwamba serikali haijaona hilo kuwa jambo la muhimu.
Ieleweke kwamba wananchi wanapokumbwa na maafa kama mafuriko, sio tu wanapoteza nyumba zao, bali pia akiba yote ya chakula. Kutarajia kuwa wananchi watajitegemea bila msaada wa serikali katika mazingira kama hayo ni kuwaonea.