Serikali imeanza kutekeleza hoja ya CAG ya kulipa fidia wakazi wa Kipunguni kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege JNIA

Serikali imeanza kutekeleza hoja ya CAG ya kulipa fidia wakazi wa Kipunguni kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege JNIA

Chikuvi2021

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2021
Posts
491
Reaction score
551
CAG kwenye ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha 2020/2021 miongoni mwa mambo mengine, alitoa hoja ya ukaguzi wizara ya Ujenzi na Uchukuzi -Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania ya kulipa fidia kwa wakazi wa Kipunguni A, Kipawa na Kigilagila waliofanyiwa uhakiki na tathamini miaka ya 1994-1997 -Lakini wakazi wa Kipawa na Kigilagila walipewa fidia mwaka 2011 kwa tathamini ya nyuma.

Serikali tayari imeshajenga terminal 3. Wananchi wa Kipawa na Kigilagila walipunjwa, lakini kwa uzalendo wao, walipisha ujenzi wa terminal 3.

-Serikali iliwazuia wananchi wa Kipunguni A kuendeleza au kufanyia matengenezo nyumba zao. -Kwenye hoja zake za Ukaguzi kwa mwaka 2020/2021 1. CAG Kichere alipendekeza Serikali ilipe fidia kwa wakazi wa Kipunguni A kupisha upanuzi wa JNIA 2. CAG alipendekeza Serikali ilipe fidia (nyongeza ya 6% kwa kila) kwa wakazi wa Kipawa na Kigilagila ambao wamehamishiwa Kigogo Fresh, Zavala, Kinyamwezi na Nyeburu, lakini wengi wao wameshindwa kumalizia kujenga nyumba zao.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAG madai hayo yaliongezeka kwa asilimia 301 (kipindi cha ukaguzi wake). 3. CAG aliagiza Serikali kupitia Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania wakae na Mthamini Mkuu wa Serikali kupitia upya madai ya wananchi wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni A, na walipe fidia stahili, kuepusha kuongezeka kwa gharama.

Serikali ya awamu ya sita ya mama Samia imefanya tathamini kwa nyumba za wakazi wa Kipunguni A na juzi Ijumaa tarehe 6 July 2023 Waziri wa fedha Dr. Mwigulu Nchemba, Naibu Spika Na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Hassan Zungu, Mh Bona Kamoli Mbunge wa Segerea na viongozi wengine wa chama na Serikali walihudhuria kwenye mkutano wa Kipunguni A kutangaza kuwa zoezi la uhakiki na tathamini kwa wakazi wa Kipunguni A limekamilika na jumla ya bilioni 140 zitalipwa kwa wakazi wa Kipunguni A kuanzia Mwezi August 2023.

Serikali ya awamu ya sita ipewe maua, Lakini wananchi wa Kipawa na Kigilagila, Kigilagila ambao nyumba zao zilivunjwa kupisha ujenzi wa terminal 3 na wao walipwe asilimia 6 kama alivyo shauri CAG ili kufunga hoja ya ukaguzi. Ninawasilisha.
 
Mama yupo vizuri tu Ila kwenye bandari ndo ametukosea
Ni uelewa tu unatusumbua wala mama hajakosea nenda Israel mwaka jana wao wameiuza kabisa bandari yao Haifa port kwa Adani group kwa bilioni 1.2 USD .unataka kuniambia waisraeli hawawezi kuijenga nchi yao?
Screenshot_20230709_211457_Google.jpg
 
Mama kanyaga twende tumechelewa sana
Mama yupo vizuri sana.Lakini awe mwangalifu na wasaidizi wake. Kwa mujibu wa hoja ya Ukuguzi wa miradi ya maendeleo ya mwaka 2020/2021 CAG alisema wananchi wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni A walipwe fidia zao kwa maana kwa kipindi cha miaka 23 ya uchelewashaji wa kufanya malipo stahiki deni limeongezeka kwa shs22.35 bilioni na kufika shs29.78 bilioni . Wasaidizi. wa Rais, baada ya kufanya uhakiki na uthamini kwa nyumba za Kipunguni A,wamekuja na deni la shs 140billioni? Ni Jambo jema kwa wananchi kupata fidia stahiki. Lakini, isije ikawa malipo halali yatakayolipwa wananchi ni pungufu ya hayo mabilioni(sehemu kubwa ikawa malipo hewa).
 
Hadi sasa tuaingia mwezi wa 9 hakuna malipo,kuna mchezo unachezwa na Wizara ya Fedha au TAA. iko kazi nchi hii. wanamwangusha mama kwa kila mbinu.
 
-Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya viwanja vya Tanzania 26 February 2025 aliitisha Mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kuwa zoezi la kulipa fidia kwa wakazi wa kipunguni litaanza Machi 2025.
-Na jumla ya 143.6 billion zitalipwa kutoka shs7.7 billion ambazo wangelipwa kwa mujibu tathimini ya 1997 ilipofanyika.
-Katika maelezo yake Mkurugenzi Mkuu wa TAA amesema ongezeko la mabilioni ni kwa sababu tathimini ya 2023 wameweka na thamani ya ardhi.
-Tunashukuru kwa Serikali kupitia TAA kulitekeleza hoja ya CAG ya 2020/2021 japo kwa kuchelewa
-Kwa mujibu wa CAG ,matakwa ya kanuni ya 13(3) ya Ardhi uhakiki wa thamani ya fidia ya Ardhi (2001) ilifanyia marekebisho ya riba ya 6% kwa mwaka.
-kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo mwaka 2020/2021 tunamnukuu "Marudio ya tathimini yalizalisha thamani mpya katika deni la awali na kufika shs29.78 billion ikiwa ni ongezeko la shs22.35 billion sawa na asilimia 302 ikilinganishwa na deni la awali"
-Lakini ikumbukwe kuwa mradi wa upanuzi wa JNIA ulihusisha wakazi wa Kipawa,Kigilagila na Kipunguni A.
-Kutokana na uharaka wa kupanua Terminal 3 wakazi wa Kipawa na Kigilagila walilipwa kwa viwango vya 1997 mwaka 2011 bila kuweka riba ya 6% kwa mwaka kama ilivyoainishwa kwa Sheria/kanuni ya 13(3) ya Ardhi uhakiki wa thamani ya fidia ya 2001.
-Viongozi wa Serikali waliwahakishia wakazi wa Kipawa na Kigilagila kuwa Serikali yao sikivu italipa ongezeko la riba ya 6% siku za mbeleni.
-Baadhi ya wakazi wa Kipawa na Kigilagila walipanga kufungua kesi, lakini baadae waliondoa mahakamani baada ya kuhakikishiwa kulipwa mapunjo.

Ushauri
-Serikali (TAA) iwalipe riba ya 6% kwa mujibu wa matakwa ya kanuni ya 13(3) ya mwaka 2001 kwa wakazi wa Kipawa na Kigilagila ambao walifanyiwa valuation 1997 na kulipwa fidia yao 2011 miaka 15plus baada ya tathimini.
-Serikali itekeleze hoja ya CAG kikamilifu badala kutekeleza nusunusu
-Kwenye hoja ya CAG baada ya kufanya ukokotoaji kwa mujibu wa Sheria na kanuni alibaini kuwa Serikali ilipaswa kulipa shs 29.78 billion kwa wakazi wa Kipawa Kigilagila na Kipunguni badala ya shs 22.35 billion ongezeko la asilimia 302 kutokana na ucheleweshaji.
-Lakini Leo watalaam wetu wanasema gharama zimefika shs143.6 billion na hapo wakazi wa Kipawa na Kigilagila hawapo.
Hili ongezeko la Zaid ya shs 100 billion ndiyo gharama za ardhi ya Kipunguni A peke yake
-CAG aliagiza TAA washirikiane na Mthamini Mkuu wa Serikali kufanya uhakiki wa madai haya,je pande hizi mbili zimekutana.

Maombi
-Mheshimiwa Rais tunaomba uingilie kati na sisi wakazi wa Kipawa na Kigilagila walipwe stahiki zao waweza kuezeka nyumba zao
-na ikikupendeza CAG afanye pre-audit ya malipo ya fidia kuepuka kulipwa wakazi hewa.
 
Back
Top Bottom