Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Bei ya jumla ya Sukari ni Tsh 2800/= kwa kilo moja, hii ni kwa DSM, lakini katika hali ya kushangaza serikali inawataka wafanyabiashara wa reja reja waiuze kwa Tsh 2600/= kwa kilo moja, hili jambo halitawezekana hata kwa mtutu wa bunduki, hivi sasa sukari madukani imefichwa na wafanyabiashara ili kuepuka hasara ya kijinga.
Hali hii imejitokeza kwenye biashara ya Barakoa, serikali iliacha box lenye barakoa 50 (surgical mask) kupanda kutoka 8500/= hadi 120, 000/= halafu leo inatangaza barakoa moja iuzwe kwa Tsh 1500/=, hili jambo halitawezekana kamwe kwa sababu hakujawahi kutokea bidhaa iliyonunuliwa kwa laki na 20 iuzwe elfu 75, hii ni biashara kichaa, vinginevyo na hizo barakoa nazo zitatoweka mubaki kuvaa barakoa za vitenge kama alivyoshauri RC wa DSM Makonda.
Kwa ufupi sana ni kwamba Wizara ya viwanda na biashara ni kama haina Waziri, ni heri enzi za Mwijage kuliko sasa.
PIA SOMA:
Serikali yatangaza bei ya kikomo ya Sukari; ipo kati ya Tsh. 2,600 na Tsh. 3,200 kwa kilo kutegemea na Mkoa - JamiiForums