Serikali imeiuza Kariakoo kwa Wachina

Mimi nataka nifahamu hawa wanaoandika kuhusu wachina. Lini kashawahi kununua bodhaa kutoka mkononi mwa wachina lini?
 
Jay one muelekeze bila matusi atakuelewa vizuri tu mkuu wangu..
 
Wafanya biashara wa k/koo walikua wanasifika kwa wizi asee sio winga wala wenye mitaji mikubwa ukiingia store wanangalia sura na lafudh wakikubal wakuj unapigikaa kinyama ata kam sio wakuja unapewa bei za kishenzi sana yaan bishaa ya 10k wanakupiga kwa 20&25k mpaka walip ingia wachina bidhaa ya 10k wanauza 10k bila kona kona watu wanatafuta unafuu mzee. Wangejielewa wafanya biashara wa kizawa mapema watu wasinge enda kwa wachina ila wizi ndo umewakimbiza so sio lawama za mchina wala serikali ni wafanya biashara wenyew
 
Umeongea point ya msingi sana. Halafu ni ujinga tu umewajaa na ubinafsi kushindwa kuelewa kuwa biashara ni kuongeza uchumi na Pato la taifa. Leo hii watanzania wanaofanya kazi china ukiambiwa utashangaa lakini hapa wamekuja kidogo watu wanaanza majungu .
 
Kwahiyo hautaki Wananchi tuuziwe bidhaa na mchina kwa Bei ya chini? Wanyonyaji wakubwa nyie. Na wewe shusha bei kama unaona haupati faida unayoitaka nenda kalime biashara waachie wahindi na wachina.
 
Mimi nataka nifahamu hawa wanaoandika kuhusu wachina. Lini kashawahi kununua bodhaa kutoka mkononi mwa wachina lini?
Bora uwaulize mkuu .maana mtu wa mwisho wala hapati unafuu wowote..eti wao wanaona winga atateseka.winga ateseke kwa lipi sasa wakati anapata wigo kubwa la kupata faida.maana yeye Hana Kodi yoyote
 
Bora uwaulize mkuu .maana mtu wa mwisho wala hapati unafuu wowote..eti wao wanaona winga atateseka.winga ateseke kwa lipi sasa wakati anapata wigo kubwa la kupata faida.maana yeye Hana Kodi yoyote
Kuna trend inaendelea alafu haina kitu, sisi watanzania walalamishi sana. Ndio maana maisha yetu hayana furaha tulio wengi.
Hivi wachina wanakua exposed na hatuwaoni. Research ipi imewahi fanywa kuonyesha wachina wakiuza bidhaa kkoo.
 
Sikatai bali wachina wanachukua kila kitu
Mimi sina shida na hao wachina wasio kuwa kwenye mifumo ya serikali kama ppp au mikataba ya kiserikali...wachina wabaya ni wale wenye kushikana mikono na viongozi wa serikali....hao wa Kariakoo watawasaidieni nyinyi pia baadae kujua njia ya kufanya biashara kama wao.
 
😆 😂 mnaotoa vibali ni nyie, Nida mnatoa nyie, simcard nyie, sasa mnalalamika nini?
Eti serikali iangalie hili
Hivi unaweza kuingia nchi tena kwenye uso wa jiji ukafanya biashara bila kibali?

Badala mjilalamikie wenyewe kwa njaa zenu, mnawatwisha mzigo Wageni

Mjitafakari ipo siku mtauza jiji lote au nchi kabisa kwa njaa zenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…