Ukwelinasema
JF-Expert Member
- Feb 10, 2021
- 733
- 928
Na hii ndologistic ambayo watu hawaelewizwewe ukileta mali hapa unapigwa ushuru mrefu hujalipa kodi bado manispaa sijui ulinzi afu bei ulioipanga sokoni anaingia mchina anauza bei aliokuuzia kiwandaniWinga haumii chochote mkuu .wanaoumia ni wafanyabiashara wenye mitaji mkubwa
Maana mchina kakuuzia vitu toka kiwandani kwake ili uje uuze nchini.na yeye anakuja nchini tena anakuja kuuza kwa bei ya chini tena Hadi mikoani kwa wateja wadogo.wewe utauza wapi?
Nina wazungumzia ni wageni wanao ishi kihalali. Hizo movements unazo sema za kibaguzi ukiwa ulaya ni kitu cha kuishi nacho. Serikali huwa ina waa assure nyie wageni walio halali usalama wenu na kuwahimiza kuendelea na shughuli zenu. Hata Trump anawatimua wale illegal immigrants tu.Huko wapi kuna movement kubwa England ya kupinga wageni na waamiaji haramu
Marekani taifa lenye uchumi mkubwa wanalalamikia wageni nenda ujerumani afd chama cha mrengo wa kulia kinapinga wageni
Kama hizo nchi kubwa duniani zinapinga wageni kwanini ni kosa kwa Tanzania
Unahukaka wahindi ukiowataja wana uchungu na TZ, Hao ni wawekezaji tu ukiwatibua wananyanyuka kama alivyofanya manji. Wana network kubwa sana nje ya nchi kuliko hata TZ mababu na jamaaa zao wapo indiaHapa Tanzania kuna Waarabu na Wahindi wenye lineage kubwa kukuzidi wewe hapo. Utakuta hata baba yake babu yako humjui.
Mansoor Daya mwaka 1962 kaanzisha kiwanda cha kwanza cha kutengeneza madawa ya binadamu hapa Tanzania. Kabla na baada ya hapo alikuwa Mtanzania hadi umauti unamfika 2024.
Kina GSM baba yao kaanza biashara mwaka 1955 na bado wapo.
Mzee Dewji kaanzisha METL miaka ya 1970s na bado yupo.
Mchina gani ana ukoo Tanzania vizazi vinne hata vitatu?
Winga anapata shida gani mchina akiwa na store kariakoo hebu tupe point mojaMawinga mishipa imewatoka hatari!! Kama mwafulani!! Hahahah!!
KAZI ni kipimo cha utu
Sawa, Wachina ndio wana uchungu na Tanzania si ndio?Unahukaka wahindi ukiowataja wana uchungu na TZ, Hao ni wawekezaji tu ukiwatibua wananyanyuka kama alivyofanya manji. Wana network kubwa sana nje ya nchi kuliko hata TZ mababu na jamaaa zao wapo india
Umeongeza point ya muhimu sana.Jifunze namna ya kuishi nayo hiyo system inga mbinu zao ama sivyo jiunge nao mshirikiane kibiashara. Hii ya mwisho nadhani ni ngumu kwani sisi Watanzania ni wavivu na wezi kwa ufupi si waaminifu..
Haiwezekani Kariakoo wachina wanaishi kama kwao.
Mbaya zaidi hawalipi kodi ipasavyo. TRA haina kanuni za asiye raia kulipa kodi kama mzawa
Hii ni sawa tu na kusema Kariakoo imeuzwa
Sawa, Wachina ndio wana uchungu na Tanzania si ndio?
Tanzania tunapata uhuru tulikuwa na Wahindi 110,000 ila wakaja fukuzwa, ondoka na kuhama baada ya Nyerere kuleta ujamaa. Wahindi kwa sasa ni wachache kuliko mwaka tunapata uhuru, walitakiwa wawe kwenye milioni moja na point ila walikimbia mazingira magumu ya nchi.
Similarly na hawa Wachina sio ndugu zetu, watanyonya kisha waache mashimo. Waje kuwekeza ila sio kuuza kuanzia pilipili kichaa, umachinga, kumiliki ardhi na migodi.
Kuna mchina atakupa mzigo bila pesa?Winga anapata shida gani mchina akiwa na store kariakoo hebu tupe point moja
National interests ni muhimu kuliko ujamaa na kutokuwa mbinafsi. Hao Wachina wenyewe wana sera za kuwekeza kwao na lazima uzifuate.Kwani mchina akiuza pilipili kuna shida? Mbona tunakua wabinafsi hivyo mkuu!
Nimekuambia mkulima hauwezi kujua habari za biashara na changamoto zake.Kama kilimo ni chepesi, toka na wewe ukalime. Siyo kukaa hapa kulialia
Hehehe.......Ngoja nichekeHaiwezekani Kariakoo wachina wanaishi kama kwao.
Mbaya zaidi hawalipi kodi ipasavyo. TRA haina kanuni za asiye raia kulipa kodi kama mzawa
Hii ni sawa tu na kusema Kariakoo imeuzwa
Mkuu habari, hivi unaweza kuingia kwenye nchi ya mtu na kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ndani ya mipaka ya hiyo nchi?Acha kulegeza makalio dogo. Pambana ufanye biashara, hizo longolongo hutoboi popote.
Angalia Mchina anafanya nini nawe iga
Wachina wanafanya nchi ya kigeni kadri ya mazingira waliyoyakuta. Wamekuta sheria ziko loose wanapita humo humo.Mkuu habari, hivi unaweza kuingia kwenye nchi ya mtu na kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ndani ya mipaka ya hiyo nchi?
Why umpangie mtu auezeje hakuna mwenye wivu, ukiona mtu anakuchukia hizo ni feedback za matendo yako yaani hisia hazidanganyi Bali akili inadanganya.Mkuu kitu kama hujui ungenyamaza Tu
Hivi bakhresa anaezalisha ngano akianza kuuza chapati nyumba kwa nyumba huoni kuna madhara kwa watu maelfu wanaouza chapati?
Mchina ana kiwanda yeye auze kwa agent .agent auze kwa mtu wa jumla .yaani kinachotakiwa ni biashara ifate mkondo wake.wala winga hausiki hapa
Tatizo huku mna wivu na matajiri WA kariakoo
Sheria za uwekezaji nchini Tanzania ziko wazi kabisa: mgeni anayetaka kufanya biashara hapa ni lazima apitie TIC na awekeze kwenye miradi mikubwa kama viwanda, uzalishaji, au huduma za kimkakati. Lengo la sera hizi si kubana mtu, bali ni kulinda soko la ndani, kukuza uchumi wa taifa, kuleta ajira, na kuongeza mapato ya kodi serikalini. Tunapowaruhusu wageni kuingia kwenye biashara ndogondogo kama kuuza sokoni au kuzungusha bidhaa mitaani, tunaharibu mfumo wa kiuchumi na kukiuka misingi ya sheria za uwekezaji.Why umpangie mtu auezeje hakuna mwenye wivu, ukiona mtu anakuchukia hizo ni feedback za matendo yako yaani hisia hazidanganyi Bali akili inadanganya.
Jiulize why mtu akuchukie yaani from nowhere akuchukie.
Imagine Kuna memory kadi ya 128gb nimeletewa na mchina akaniambia nimrudishie aliyonunulia kwao ambayo ni 15k nikashangaa mno nikamwambia kuwa hapa ni 87k akashangaa mno.
Kuna jamaa aliagiza Ile huwaei akalipa 400k iyo simu hapa inauzwa muda huo sh 1.6M.
So why mtu asifurahie kupata unafuu yaani watu wengi mno hawajui biashara,
Biashara ni mzunguko usikomalie faida kubwa mno,
Mie nikiagiza kitu cha laki nne nikipata hata faida 25-50 inanitosha mno Sina haja ya kuuza 1.6M.
Tulia Sasa si mlikuwa mnafurahia acha Sasa ivi na wengine wafurahie.
Pia hakuna tajiri hapo kariakoo , hebu niambie Kuna watu wangapi Wana miliki Dola bilioni moja kwenda juu.
Hao watu mnaowaona matajiri wakienda huko nje wanapoteana wanakuwa Kama machinga tu hapa bongo kwa nje.
Ni sawa na Yule jamaa ambaye ama duka Kijijini ana kigari ama boda yake basi anavimba anajiona yu tajiri kwa walimu wa primary au wakulima Ila akija hata mjini kidogo like bukoba mjini hata hakuna anayejua kuwa Kuna mtu mwenye hela.
Dar ni Kijijini MNo kulingnisha na huku mjini Stockholm.
Sema unamiliki dola laki 2-6 Ila unavimba na wewe unajiona ni tajiri .
Matajiri Africa wapo wachache like baresa, mo, Dangote wenye Dola bilioni moja and upward Ila hizo hela zako hata huwezi miliki mjengo New York Manhattan Wala hata sikuelewi Kama unazo hela.
Yaani unazo hela za kubadilisha mboga na wewe unajiona una hela.
Watu wanatoa misaada mpaka bilioni kadhaa za kitanzania Wana hela Sasa wewe hata kutoa msaada milioni moja ama laki moja ni kipengele
Swali la "kwani Mchina akiuza pilipili kuna shida?" linaonekana rahisi, lakini lina mzizi mpana wa kisera na kisheria. Sio kwamba kuna shida kwa mtu kuuza pilipili, bali ni nani anayeuza, chini ya utaratibu gani, na kwa madhumuni gani. Sheria za Tanzania kuhusu uwekezaji haziruhusu raia wa kigeni kufanya biashara ndogondogo kama kuuza pilipili sokoni, kuuza mitaani au kufungua fremu ndogo hizi ni biashara zilizotengwa kwa wazawa kwa lengo la kulinda ajira na soko la ndani.Kwani mchina akiuza pilipili kuna shida? Mbona tunakua wabinafsi hivyo mkuu!
Ni kweli kabisa kuwa dunia ya sasa imeunganishwa sana kiuchumi, na hatuwezi kukwepa kutumia bidhaa kutoka nje, ikiwemo China. Lakini hoja ya msingi hapa si chuki wala uonevu kwa wageni ni kusimamia sheria, kulinda soko la ndani, na kutetea ajira kwa Watanzania wa kawaida. Kama taifa, hatuwezi kuacha kila mtu afanye anachotaka bila kufuata sera na taratibu tulizojiwekea kwa faida ya wote.Acheni wageni wapumue kidogo, mmewakalia kooni utafikiri tutaishi milele, hapo kwa asilimia kubwa unatumia vifaa vya mchina