Serikali imejiandaa kuhudumia maabara zinazojengwa ?

Serikali imejiandaa kuhudumia maabara zinazojengwa ?

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,296
Reaction score
18,027
Kumekuwa na kelele nyingi kuhusu ujenzi wa maabara ulioamriwa na Rais Kikwete. Mwelekeo unaomnyesha kuwa tafsiri ya maabara kwa upande wa serikali ni majengo. Kwanza sipingi wazo la wananchi kuchangia maendeleo yao lakini hili la maabara limekuwa kero kwa wananchi mabao wanalazimishwa kuchangia hadi kuwekwa ndani baadhi ya maeneo.

Lazima tutambue kuwa maabara si majengo pekee. Lazima kuwe na wafanyakazi (sio waalimu), yaani watu (Laboratory Technicians) wa kuendesha hizo maabara. Je hao watu wapo? Hao wanasomeshwa kufanya kazi hizo. Hata katika shule kongwe za serikali ni wachache sana.

Swali lingine muhimu ni vifaa na madawa ya kutumia kwenye hizo maabara. Serikali imejiandaa kwa hili? Kwa mfano kwenye maabara za kemia, kunahitajita vitu kama beakers, pippetes, burners pamoja na kemikali kama sulphuric acid nk. Uwepo wa vitu hivi unahitaji Laboratory Technician kuvitumia na kutayarisha na si kazi ya mwalimu wa somo husika. Mwalimu hana utalaamu wa kuchanganya madawa hayo!

Serikali yetu hii itatoa fedha kununua vitu hivyo kama inashindwa kununua madawati? Nina wasiwasi watu watahenyeshwa na mwisho wa siku hizo maabara zitakuwa ni white elephants tu. Kwanza ujenzi wake hauwezi kuwa na sawa na darasa la kawaida. Ni vyumba vyenye design na mahitaji maalumu kabisa. Sina uhakika kama yote haya yamezingatiwa.

Inaelekea mheshimiwa alitamka tu kuwa hadi tarehe fulani kila shule iwe na maabara lakini hakuna mwenye ujasiri wa kumweleza kuwa kuna mambo kadhaa ya kuzingatiwa ili kufanikisha malengo hayo. Pia tukumbuke kuwa kila somo la sayansi linahitaji maabara yake. Ya kemia haiwezi kuwa ya fizikia!

Tumeingiza mno siasa kwenye elimu na gharama zake ni kubwa mno kwa taifa letu. Mimi naona maabara zinazojengwa ni nyongeza tu ya madarasa! Ujenzi wa maabara unahitaji serikali ijipange na kutenga fedha za ujenzi, vifaa na madawa na baadaye iendelee kuzihudumia kila mwaka.
 
Wanakosa dawa za hospitali wataweza kununua lab equipment na reagents kwa shule zote, wazabuni wa kuleta chakula mashuleni hawajalipwa mwaka mzima, shule haijapata matengenezo for the past 20 years maabara zilizopo hazina hata beaker wala tripod stand, nashangaa itawezekana vipi kuwa na maabara kila shule.

Mimi nafikiri bora wange dedicate shule kadhaa zijengewe uwezo wa kimaabara na ziweze kuhudumia shule nyingine za jirani na shule hizo ziwe mahali ambapo wanafunzi wa shule jirani wanaweza kufika walau mara chache katika mwezi na kufanya practicals za maana kuliko kuishia kuwapeleka wanafunzi maabara na kuishia kutoa nadharia ya practical. Sijui? Ngoja tuone itakuwaje?
 
Kwa mfano mikoa ya kusini utakuta walimu wa biology/chemistry/physics wapo wawili au watatu hapo napo maabara sijuwi zitafanyaje kazi
 
Nakubaliana na Sibonike. Ufanisi wa maabara unaanza kutia shaka kwani hata walimu waliopo hawakuandaliwa vizuri. Tembelea vyuo vya ualimu vinavyowaandaa walimu wa sayansi, utachoka!
 
Hospital hakuna dawa ya kumeza mgonjwa apone, itapata dawa za kutumia maabara kuunguza eti mnajifunza?? Labda kwa kuwa mzalendo anachukua nchi miezi10 ijayo!!
 
Sibonike

Aliyepata moja, si sawa na mwenye sifuri. Unataka uamke kesho na ukute Tanzania iko kama Marekani? Tunasonga mbele. Leo tunajenga maabara, barabara, kuweka uhuru kwa watanzania kuwafichua wachafu wachache tulionao n.k; kesho tutafanya kitu kingine chenye faida kwa watanzania wote.

Tatizo ni hawa wachache (baadhi ya watawala na wapinzani) wanaopunguza kasi yetu ya maendeleo kwa kuijichotea akiba zetu!!!
Jamani tutibue maovu na sio maendeleo !
 
Last edited by a moderator:
aliyepata moja, si sawa na mwenye sifuri.
Unataka uamke kesho na ukute Tanzania iko kama Marekani?
Tunasonga mbele. Leo tunajenga maabara, barabara, kuweka uhuru kwa watanzania kuwafichua wachafu wachache tulionao n.k; kesho tutafanya kitu kingine chenye faida kwa watanzania wote.
Tatizo ni hawa wachache (baadhi ya watawala na wapinzani) wanaopunguza kasi yetu ya maendeleo kwa kuijichotea akiba zetu!!!
Jamani tutibue maovu na sio maendeleo!!!

Tanzania haiwezi kulala leo ikaamka kesho ikawa kama USA. Lakini hiyo sababu ya kufanya mambo ovyo ovyo. Hatuwezi kuishi kama wanyama wa porini. Maabara ni wazo zuri mno lakini lazima kuwe na mipango inayoeleweka.

Hivi tunahitaji watu watoke nje ya nchi kutufundisha kufanya maandalizi? Maabara sio chumba kama darasa la kawaida. Lazima iwe mtalaam an vifaa pamoja na kemikali husika ili iitwe maabara. Waulize hao waheshimiwa kama wanajua gharama ya kuendesha maabara moja yenyewe uwezo wa kuhudumia wanafunzi ishirini kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom