The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wakuu
Wizara ya Afya imewekeza Sh5 bilioni katika ujenzi wa jengo jipya la tiba mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.
Hatua hii inalenga kuboresha huduma za matibabu ya saratani kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini na maeneo jirani.
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Akizungumza leo Jumamosi Machi 1, 2025 wakati wa ziara yake hospitalini hapo, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, amesema ujenzi wa kituo hicho umefikia hatua nzuri na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Aprili mwaka huu.
"Sisi kama sekta ya afya si washindani, bali tunashirikiana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora," amesema Mhagama.
Amesema kituo hicho kitakuwa miongoni mwa vituo vichache nchini vinavyotoa tiba ya saratani kwa mionzi, huku kikiwa na wataalamu waliobobea waliopata mafunzo kwa ufadhili wa serikali.