Serikali imetaja njia mbadala ya kumaliza ama kupunguza rushwa, ni kujenga mifumo ambayo itakuwa wazi katika utoaji wa huduma za kiserikali ikiwemo kutokutana moja kwa moja na wenye kutoa uamuzi huo, huku ikieleza ni muhimu rushwa kutamkwa kwa uwazi kuelekea uchaguzi mkuu ili kukomesha vitendo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Julai 11, 2025 wakati wakati akifungua kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano ya rushwa Afrika yanayofanyika Jijini Dodoma.
Wakati Simbachawene akitoa kauli hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amesema mwaka huu wa uchaguzi ni lazima suala la rushwa lizungumzwe kwa nguvu zote kwani linaweza kuharibu taswira nzima ya nchi.
Simbachawene amesema kuwa huduma za Serikali hazipaswi kutoa nafasi ya watu wenye kufanya maamuzi kukutana moja kwa moja na watu wenye mahitaji ya huduma hivyo teknolojia inapaswa kuchukua nafasi yake katika hilo.
Waziri Simbachawene amesema licha ya tatizo la Rushwa nchini, lakini Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwenye mapambano yake kulingana na taarifa za vyombo vya kimataifa.
View attachment 3402268