Serikali imewaibia Wamachinga?

Mnataka Bongo iwe kama Denmark ulipo, au sio? Ila usisahau hapo Posta tu, hakuna hata chombo kimoja cha kutupia taka . Vipi Denmark huko?
 
Una usingizi wewe, kwanini unatetea hata ujinga? Kwanini kila kitu unakiweka siasa?? No, hii sio sahihi
Wewe unaona sahihi walivyokua wanahatarisha maisha yao Kwa kufanya biashara chini ya transforma, pembeni ya barabara na mbele ya maduka ya watu?? Unafahamu masharti ya kupata kitambulisho Cha machinga ambacho siku hizi unajisali online?? Fatilia na utagundua hakuna machinga alieibiwa na serkali
 
Ndio maisha ya wananchi wako hayo.wangekuwa na hela wangeenda kula Hyatt regency hotel.
angalia vipato vya wananchi wako unadhani wanapenda kuwa mama ntilie au machinga?
lini serikali imetangaza machinga wote wenye elimu waende kuajiriwa?.
Achans dhana kula wapi.....wakipangwa vizuri poa tunaenda kula...ule ni uchafu mjini....zamani tulikuwa tunakula mama ntilie town sehemu zilizoandaliwa kwa mama ntilie mimi nimekula sana mama ntilie wa ferry suala sio kwenda setena au kipato mpangilio mzuri....
 
Mnataka Bongo iwe kama Denmark ulipo, au sio? Ila usisahau hapo Posta tu, hakuna hata chombo kimoja cha kutupia taka . Vipi Denmark huko?
Niko kwa Mtogole mkuu....huko Denmark uliko wewe sijawahi hata kufika!

Acha maskhara mkuu yaani mitaa ya Posta ikose "ndoo za taka dustbins"?!!!!🤣
 
Uteuzi uliishaga.
 
Ukiona mama ntilie NI wengi jua watu wasiokuwa na kazi WAMEONGEZEKA.
Zamani uliona wapo kwenye mpangilio sababu hawakuwa wengi
 
Ukiona mama ntilie NI wengi jua watu wasiokuwa na kazi WAMEONGEZEKA.
Zamani uliona wapo kwenye mpangilio sababu hawakuwa wengi
Kazi gani ?!!

Kazi zipi?!!

Sasa huko kwa mama Ntilie baada ya kula wanalipa nini na kazi hawana?!!!
 
Kabla hawajafunga mabarabara, njia za wapita kwa miguu na mitaro ya maji walikuwa ? Warudi huko walipokuwepo kabla hawajaruhusiwa kuvamia maeneo yasiyo maalum na Mpenda sifa
... eti mtu na akili zake anauliza waende wapi! Uholela huo ukiachwa maana yake yeyote popote alipo ana haki ya kujifanyia biashara popote mijini bila kuzingata sheria zilizopo. Kila mwaka maelfu kwa maelfu ya vijana wanahamia mijini na kama kimbilio la walio wengi ni kufanyia biashara mabarabarani hali itakuwaje huko tuendako?

La muhimu sheria zisimamiwe kikamilifu vinginevyo linatengenezwa tatizo la kudumu kwa kisingizio cha wanyonge! Ni aibu kwamba ilifika mahali wakajihalalishia maeneo hayo kinyume cha sheria na taratibu za mipango miji kwa kisingizio cha kulipia 20,000! Aliyebuni hili ni sehemu ya tatizo na mvunja sheria namba moja kwa suala hili la umachinga.
 
Hili la 20k lilikuwa ni kituko cha mwaka, and vitambulisho vyenyewe vilikuwa havina picha, walichokuwa wanafanya ni kuazimana tu vitambulisho pale vilipokuwa vinahitajika!! And kuna watu Bwana yule aliwatumbua kisa hawakumaliza kuuza vitambulisho vyote
 
Kazi gani ?!!

Kazi zipi?!!

Sasa huko kwa mama Ntilie baada ya kula wanalipa nini na kazi hawana?!!!
Wanaokula ni machinga,wabeba zege,makonda n.k.
Wapishi Sasa ndo hao wameamua kujiajiri sababu hakuna kazi.
Tuseme tu ukweli kazi ya mama ntilie miaka ya nyuma ilikuwa inadharaurika ila Sasa hivi mpaka wasanii na watu maarufu wanafanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…