Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Faustine Kimath, katika chapisho lake la Julai 01, 2021, anasema, mfumo wa kodi nchini Tanzania unajumuisha aina mbalimbali za kodi zikiwemo Kodi za Moja Kwa Moja (“Direct Taxes”) na Kodi zisizo za moja kwa moja (“Indirect Taxes”).
Historia Fupi ya mfumo wa Kodi Tanzania
Kwa mujibu wa chapisho la CUP London (1969), sheria ya kwanza ya kodi ilianzishwa na utawala wa Ujerumani mwaka 1897. Katika maeneo yaliyokuwa chini ya udhibiti kamili wa kisiasa wa Mjerumani, kulikuwa na Kodi ya Kichwa (maarufu kama “Hut Tax”), na hii ililenga kuwafanya Waafrika kukubali kufanya vibarua vyenye malipo na hivyo kuwafanya kuwajibika kwa utawala wa Wazungu.
Katika kipindi cha utawala wa Uingereza (1919 – 1961), pamoja na kuanzisha aina nyingine za kodi, iliendeleza kodi hii ya kichwa (ambayo iliitwa “Poll Tax”).
Napenda kujikita zaidi katika swala la kodi za Ardhi na Majengo nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ardhi yote nchini Tanzania ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Raisi kama mdhamini (msimamizi) mkuu kwa niaba ya Watanzania wote. Hii inamaanisha kuwa Wananchi wote ni wapangaji katika ardhi na hivyo wanapaswa kulipa Kodi ya Ardhi.
Kodi za Majengo (“Property Tax”) na Ardhi (“Land Rent”), zimekuwa zinalipwa kwa kiasi kidogo sana, kwani wamiliki wengi wa ardhi na nyumba hawajui umuhimu wake. Ukweli huu unathibitishwa na chapisho la Merima Ali, Odd-Helge Fjeldstad and Lucas Katera (2018), kufuatia utafiti uliofanyika Jijini Dar es Salaam na Manispaa ya Mtwara Oktoba, 2017.
Wizara ya ardhi inauza viwanja kwa bei tofauti kulingana na ukubwa, eneo, nk. Aliyenunua kiwanja anajenga nyumba yake kwa gharama zake, kila alichokinunua kwa ajili ya ujenzi analipia kodi; akifungiwa maji, umeme na labda gesi na mamlaka husika atagharamia. Huduma nilizozitaja, zinalipwa kadiri ya matumizi, na kila Ankara ina tozo mbalimbali za serikali.
Kuna kodi inayojulikana kama LIPA KADRI UNAVYOPATA (“PAY AS YOU EARN – PAYE”); ikiratibiwa na kukusanywa vizuri inaweza kuongeza mapato ya serikali, na hivyo kupunguza utegemezi katika maeneo manyonge ya kodi, ambayo yanamwangukia mwananchi wa kawaida bila kujali hali ya kipato chake. Kama ardhi na/au jengo linatumika kufanya biashara, biashara yoyote hutozwa kodi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na “PAYE”. Kwa mfano, kama amepangisha nyumba/vyumba, mwenye nyumba atapaswa kulipa “PAYE”.
Sidhani kwamba mfumo huu wa kodi ni sahihi, eti kwa sababu ulikuwepo toka enzi za ukoloni au kwa kuwa hata nchi nyingi zina utaratibu huo; kama nchi huru tunaweza kuwa na mfumo tofauti na wenye maslahi mapana ya taifa.
Nidokeze kuhusu Kodi ya Kichwa. Faustine Kimath (Julai 01, 2021), anasema, kodi ya kichwa (“Poll Tax”) iliyokuwepo toka enzi za ukoloni, ilifutwa na serikali mwaka 1969, kwani ilikuwa ikilalamikiwa kuwa ni ya kinyanyasaji. Huo ukawa mwanzo wa kuanzishwa kwa kodi nyingine mbalimbali mpaka kufikia utitiri wa kodi ambao upo hivi sasa.
Kodi ya kichwa ilibadilishwa jina, ikaitwa Kodi ya Maendeleo, ambayo ilikusanywa na halmashauri za majiji, manispaa, miji, na wilaya.
Kufutwa kwa Kodi ya Maendeleo
Kodi hii (ambayo iliwahusu zaidi wanaume watu wazima) iliendelea kuwa kero kwa watu, kiasi cha kuwafanya baadhi yao kuzikimbia kaya zao na kwenda kujificha maporini wakati maofisa wa halmashauri wakipita kuzikusanya. Jambo hili lilizorotesha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla, kwa kuwa watu wengi (hasa wa vijijini) walitumia muda mwingi kukimbia watoza kodi, badala ya kutulia na kufanya uzalishaji.
Kero hizi ndizo zilimfanya Raisi wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa, kufuta rasmi kodi ya Maendeleo, katikati ya mwaka 2000; na mpaka leo (Agosti, 2022) haijawahi kurudishwa.
Inawezekana kufuta kodi ambazo ni kero kwa wananchi
Kama Raisi wa awamu ya tatu, Hayati Benjaminpa aliweza kufuta Kodi ya Maendeleo, iliyokuwa ikitegemewa sana na Halmashauri nyingi nchini kama chanzo muhimu cha mapato, na iliyokuwepo miongo mingi toka enzi za ukoloni; basi hata leo serikali inaweza kuzifuta kodi hizi za Majengo na Ardhi.
Inawezekana watu wanaona hizi tozo ni za kawaida na haziumizi sana, lakini ni muhimu kupiga picha ya miaka mingi ijayo. Kwa mujibu wa chapisho la “EH Encyclopedia” nchini Marekani, pamoja na kodi nyingine, kodi za ardhi na za majengo zilianzishwa mwaka 1796, ambazo ziliendelea kufanyiwa maboresho kulingana na wakati na ukuaji wa uchumi. Kwa mujibu wa chapisho hili, mwanzoni mwa miaka ya 1900, wananchi wengi kutoka maeneo mengi nchini Marekani walipinga vikali tozo hizi; serikali iliendelea kuzifanyia marekebisho bila kuzifuta, lakini mpaka leo watu wengi husani wale wa kipato cha chini wanaendelea kuzipinga.
Kodi hizi zimefanya gharama za makazi kuwa ghali sana nchini Marekani, hali inayofanya watu wengi kukosa makazi na kuishi mitaani.
Makazi yaliyotelekezwa nchini Marekani (1). Chanzo: www.gettyimages.com
Makazi yaliyotelekezwa nchini Marekani (2). Chanzo: www.gettyimages.com
Makazi yaliyotelekezwa nchini Marekani (3). Chanzo: www.gettyimages.com
Mwaka 2013, nilitembelea majiji mbalimbali ya Marekani, nikajionea majumba mengi yakiwa tupu, yakiwa yameachwa na wamiliki/wapangaji, baada ya kushindwa kumudu gharama zake. Pia niliwaona watu wengi wakiishi mitaa mbalimbali ya majiji wakiomba misaada kwa kuwa hawana kazi na/au makazi.
Mtu asiyekuwa na makazi katika moja ya majiji ya Marekani (1). Chanzo: www.voa.org
Mtu asiyekuwa na makazi katika moja ya majiji ya Marekani (2). Chanzo: www.ohsoupkitchen.org
Vibanda vya wasioukuwa na makazi katika moja ya majiji ya Marekani (3). Chanzo: www.pbs.org
Serikali yetu inaweza kufuta tozo hizo, tukaepukana na aibu ya baadhi ya wananchi kukosa makazi katika kizazi hiki na/au kizazi kijacho.
Mapendekezo
Serikali ibaini maeneo mapya na ya kimkakati ya kutoza kodi, ili kumpa nafuu mwananchi wa kawaida.
Serikali iunde timu maalumu itakayohusisha watu kutoka kada tofauti, ichunguze na kubaini maeneo mapya ya kodi.
Serikali itafute wawekezaji makini wa kuwekeza katika maeneo ya kimkakati kama gesi, madini, nk. na kuhakikisha kila mwananchi ananufaika kwa namna moja au nyingine.
Hitimisho
Kodi za ardhi na majengo zinaweza kufutwa bila kuathiri mapato ya serikali.
Rejea
CUP London (1969), “Tanganyika under German Rule 1905-1912”
“eh.net/encyclopedia, History of Property Taxes in the United State”
Faustine Kimath (Julai 01, 2021), Ufahamu Mfumo wa Kodi Nchini Tanzania
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la mwaka 2000.
Merima Ali, Odd-Helge Fjeldstad and Lucas Katera (2018), “Property owners’ knowledge and attitudes towards property taxation in Tanzania”

Upvote
11