Serikali imuangalie Humphrey Polepole kwa jicho la karibu. Hana nia njema!

Serikali imuangalie Humphrey Polepole kwa jicho la karibu. Hana nia njema!

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
863
Reaction score
1,534
Kuna habari inazunguka mtandaoni ikiwa ni pamoja na humphrey pole pole mwenyewe kuichapisha kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba amevamiwa nyumbani kwake dodoma na watu wasiojulikana.

Kwangu naliona hili tukio kuwa ni tukio la kutengeneza kwa sababu kuu mbili;

1. Pole pole anatafuta huruma kwa watu
Nadhani wote tunafahamu mwenendo na msimamo wa huyu kijana kuhusu serikali ya awamu ya sita. Labda kwa msiofahamu ni kwamba pole pole amegoma kabisa kuitambua serikali ya awamu ya sita na amegoma kabisa kumheshimu Rais aliyepo madarakani hivyo tukio la leo ni la kutengeneza ili kutafuta huruma na uungwaji mkono kwa watu ionekane kwamba serikali ya awamu ya sita inamfanyia mambo yasiyofaa.

2. Pole pole analenga kuichafua serikali kwa wananchi
Kuna uwezekano mkubwa kwamba tukio la leo ni la kutengeneza ili kuichafua serikali kwa wananchi. Itakumbukwa kuwa, siku za hivi karibuni pole pole amewahi kunukuliwa akiwatuhumu viongozi kuwa ni 'wahuni'. Hivyo katika kuhakikisha anaipa mashiko hoja yake ya 'uhuni' anaosema ameamua kutengeneza tukio la leo ili kutuma ujumbe kwa wananchi kwamba 'uhuni' aliosema upo na hivyo wananchi waamini maneno yake na kukosa imani na serikali yao.

Na kama kweli tukio hili limetokea basi tunaomba pole pole atuonyeshe footage za cctv camera za tukio zima na kama hiyo nyumba haijafungwa CCTV camera atwambie wakati tukio linatendeka nani alikuwepo nyumbani na aliambiwa kitu gani na wahusika wa tukio hili? Alipigwa? Pole pole atuambie.

Kwakuwa pole pole mwenyewe amekusudia kuripoti jambo hili kwenye vyombo vya dola ni jambo jema kwani ndio utakuwa mwanzo mzuri wa jeshi la polisi kufanya uchunguzi na endapo itabainika kuwa ni tukio la kutengeneza, tunaomba kijana huyu ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria ili liwe fundisho kwa wale wote wenye nia ovu ya kuchafua serikali ya awamu ya sita kwa maslahi yao binafsi.

Muwe na siku njema.
 
Kuna habari inazunguka mtandaoni ikiwa ni pamoja na humphrey pole pole mwenyewe kuichapisha kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba amevamiwa nyumbani kwake dodoma na watu wasiojulikana...
Si uende kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na wewe uwaambie ilo tukio si la kweli ili uweze kuwasaidia Polisi kwenye uchunguzi wao
 
Mwacheni Polepole afanye anayofanya, anatumia uhuru wake kikatiba kwa anayofanya kama amevunja sheria semeni. Huo ndio uhuru ambao kila Mtanzania anao. Mpingeni kwa hoja na sio viroja.

Kama mna ushahidi nyumba yake haikuingiliwa na vibaka toeni ushahidi wenu kwa Polisi ambako yeye kapeleka malalamiko yake.
 
Si uende kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na wewe uwaambie ilo tukio si la kweli ili uweze kuwasaidia Polisi kwenye uchunguzi wao
Ni njia ya kutaka kuwapoteza watu maboya kuhusu kesi ya Mbowe. Waswahili wanasema miluzi mingi humpoteza mbwa. Hii ina maana kuwa kuna watu (japo sio wote) watakuwa busy kufuatilia habari za "Mr Taratibu" na kusahau zile za Mbowe.
 
Ushahidi wa nyumba kutoingiliwa na vibaka unaweza kuwa upi?
Mwacheni Polepole afanye anayofanya, anatumia uhuru wake kikatiba kwa anayofanya kama amevunja sheria semeni. Huo ndio uhuru ambao kila Mtanzania anao. Mpingeni kwa hoja na sio viroja.

Kama mna ushahidi nyumba yake haikuingiliwa na vibaka toeni ushahidi wenu kwa Polisi ambako yeye kapeleka malalamiko yake.
 
Kuna habari inazunguka mtandaoni ikiwa ni pamoja na humphrey pole pole mwenyewe kuichapisha kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba amevamiwa nyumbani kwake dodoma na watu wasiojulikana...
Kamchukulie RB mkuu
 
Mshaanza kumfanyia ujinga wenu
IMG-20211212-WA0218.jpg
IMG-20211212-WA0217.jpg
 
Hii ni sawa na yule kijana wa Kigoma aliejiteka mwenyew, afu baadae ikalalamikwa kuwa katekwa.
Ndio maana nasisitiza uchunguzi ufanyike isijekuwa slow slow naye ameiga nyendo zil zile kutafuta kiki na umaarufu wa kisiasa
 
Back
Top Bottom