Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Serikali inatakiwa iwe na muongozo mpango miji wa taifa zima wenye ramani wa miaka angalau 25 kuonyesha wapi itajenga barabara za lami, wapi itajenga reli, wapi itajenga mwendokasi, wapi itajenga vituo vya mabasi, wapi itajenga viwanja vya mpira, wapi itajenga stendi n.k
Huo muongozo ndio ungekuwa nyenzo ya kuzuia watu kujenga maeneo ambayo miondombinu itapita halafu baadaye kubomelewa na kuibuka sarakasi za fidia. Kama hakuna huo muongozo basi tumechelewa sana lakini hata hivyo unaweza kuandaliwa kuepusha ujenzi katika maeneo ambayo bado hayajajengwa,.ni rahisi zaidi kulipa fidia ya shamba kuliko nyumba ya mtu.
Pia huo muongozo ndio ungeepusha nchi hata na hasara za bomoa boma za miondombinu yake yenyewe iliyojengwa kwa mabilioni kama ya lami ili kuongeza miondombinu mengine kama ya mwendokasi na reli.