Serikali Inabagua vyuo Vikuu Binafsi??

Serikali Inabagua vyuo Vikuu Binafsi??

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,523
Reaction score
87
Hivi Karibuni Serikali ilipata Pesa toka benki ya Dunia kwa ajili ya Kuboresha vyuo vikuu mbalimbali Nchini Tanzania, Lakini hata hivyo pesa zimepelekwa kwenye Vyuo vya Umma tuu, Yaani vyuo vya serikali, yaani, Chuo Kikuu cha Ardhi,Chuo Kikuu cha Dar-Es-Saam (UDSM), Chuo Kikuu huria Cha Tanzania,(OUT) Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lakini kwa mujibu wa Mmoja wa wajumbe katika tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) Ambaye ni Askofu Na Mkuu wa Chuo Kikuu cha St Augustine university amesema kuwa pesa hizo ni Mkopo toka Benki ya Dunia hivyo ni Bora zigawanywe sawa na Vyuo Binafsi.

Je, wadau hivi ni sawa au vipi maana ukitazama kwenye vyuo ambavyo zimesajiliwa Tanzania ni kama 32 hivi, Je pesa hivi ni sawa wapewa watu wanaosoma kwenye vyuo vya umma tu??

Je, hivi vyuo vya binafsi zinatoa huduma kwa wakina nani?? tuomba Waziri wa elimu wa Juu asema kuwa ana maana gani kutoa pesa kwenye vyuo vikuu vya umma wakati huo watu wote wanalipa pesa hizo?? je watu kama wanasoma Tumaini, Ruaha, Mwenge wafanye nini?? Je Huu sio uonevu kwa watu kama hawa, je kama kuboresha Mazingira katika Vyuo vyetu basi ni Kote maana watu wanatoak Huduma kwa Watanzania, jamani naombeni Majibu.

Elimu wa Wote Bila Ubaguzi
 
Kwani hivi vyou binafsi wao wakipata misaada/Mikopo toka nje je pia huwapa vyuo vya serikali??

Kwa nini serikali iwajibike kugharamia vyuo binafsi??
 
Last edited:
Kwani hivi vyou binafsi wao wakipata misaada/Mikopo toka nje je pia huwapa vyuo Binasfi??

Kwa nini serikali iwajibike kugharamia vyuo binafsi??

Mzalendo,
Hapa tunazama Serikali kama BABA mwenye pesa za kuwatunza wanae wadogo ambao hawajaweza kujitegemea. Vyou binafdi vinafanya juhudi kubwa mpaka kuonekana kama chuo kikuu, mara kiombe msaada Marekani, mara serikalini , mara nyingine hata waumini wa dini fulani wanachangia.

Tunaamini Serikali ina mkono mrefu, inaweza kugharimia au kutoa ruzuku kwa vyou binafsi na Serilkali. Inapopata msaada, inatakiwa isaidie vyuo vyote na hasa vyou binafsi ili vijitegemee na kuzaa matunda mazuri.
 
Katika Nchi zilizoendelea huwa wanatoa ruzuku kwa vyuo binafsi kwa ajili ya kuendesha vyuo hivyo, Nchi kama Marekani kuna mikopo kabisa na ruzuku toka kwa States husika kwa ajili ya kutoa pesa kwenye vyuo hata kama ni binafsi maana suala la elimu ni muhimu sana katika maendeleo ya taifa.

Je, kama ni pesa za walipa kodi ambazo wewe na mimi tutatoa itakuaje, Leo katika vyombo vya habari Tanzania vimetawala kwa Maskofu kupinga suala la kufutiwa kodi katika shughuli zao. Je vipi na Hizi taasisi za Dini?? kama Shule, Vyuo na Hospitali?? Kutakuwa na pengo kubwa sana kati ya Vyuo vya umma na binafsi katika Kutoa Elimu Tanzania.

Lazima kwa serikali kama Mlezi Kutoa pesa kwa ajili ya kulipia hata baadhi ya vitu katika Elimu ya Juu kwenye vyuo hivi binafsi..!! Kuna utaratibu ule uliotumia kama wa kutoa baadhi ya mishahara ya wafanyakazi kwenye hospitali za Dini na kupewa pesa toka serikani kwa ajili hiyo. Maana mchango wa Vyuo hivi ni mkubwa sana katika nchi Yetu.

Hivi basi itakuwa jambi nzuri sana kama serikali ikavipa pia pesa hizo na mkopo toka Benki ya Dunia maana wote watakuja kulipa sio Vyuo vya Umma tu..

Elimu kwanza mengine baadae
 
Jukumu ya huduma za jamii ni la serikali!

Serikali wanaweza kuwajibishwa ktk kura kila miaka 5 kama hakuna hizi huduma au kama ni mbovu!

Je mashirika ya Dini wanawajibika kwa nani kama huduma zinakuwa mbovu??

Nchi kama China, Norway na Cuba..watoto wote au 95% kusoma shule za serikali na hata watoto wa mawaziri pia husoma huko2!

Pia tiba..hospitali nzuri inabidi ziwe za serikali..kwa vile serikali hukusanya kodi!

Tungeiwajibisha serikali ifungue Chuo Kikuu kila Mkoa!

Kwa nini serikali iwajibike kwa vyuo binafsi??? Why???
 
Hivi Karibuni Serikali ilipata Pesa toka benki ya Dunia kwa ajili ya Kuboresha vyuo vikuu mbalimbali Nchini Tanzania, Lakini hata hivyo pesa zimepelekwa kwenye Vyuo vya Umma tuu, Yaani vyuo vya serikali, ...
Yeah, serikali inatoa huduma kwa vyuo vyake, yaani vya serikali, na bahati nzuri umejipa jibu mwenyewe. Ni vyema ungezungumzia misamaha ya kodi kwa huduma fulani (ambayo serikali imeiondoa juzi kwa taasisi za kidini, ambazo pamoja na huduma nyingine, zinamiliki vyuo binafsi). Nadhani kwa misamaha ya kodi katika kuagiza vitabu, madawa etc, ungeeleweka zaidi. Lakini kwa serikali kutoa fedha zake cash kuzipa taasisi binafsi, duuh!! Hata hivyo tayari vyuo binafsi vinafaidika kupitia bodi ya mikopo Elimu ya juu (HESLB), kwani bila mikopo hiyo, wanafunzi wangekuwa wachache sana, na ndio maana vyuo binafsi vimeongeza ada ya masomo vikijua wanafunzi watakopeshwa tu!
 
Opaque,

Ndugu yangu hata wewe unaweza kuwa una ndugu anasoma huko, pia haya mashirika yanachofanya ni kutoa huduma ndio maana hata zile shule wakati ule wa Nyerere aliweza kutaifisha na kurudisha serikalini, Hivyo Jukumu la kutoa Elimu ni la Serikali na sio hizi taasisi.

Hivyo wana kila wajibu wa kudai wapewe nao maana zote ni za Tanzania, Je kama Chuo cha Kislamu Morogoro watatoa wapi pesa za kuendeshea chuo katika hali ya ushindani kama hivi bila serikali kutoa pesa hata za Ruzuku kama ilivyo kwenye vyama vya Siasa, Mbona Wao pia wanapata faida kubwa,Mimi sijakubali kutoa misamaha ya kodi tu kwenye vitabu hata ruzuku kila mwaka kupitia kwenye tume ya vyuo Vikuu Tanzania (TUC) ingebidi wapewe fedha wao na kutoa kwenye vyuo hivi.

Je na haya mambo ya kufutiwa kodi ndio watakuwa katika wakati mgumu sana katika kuendesha shule zao na vyuo vyao
 
Back
Top Bottom