Serikali inadhibiti vipi maduka ya vifaa vya magari vilivyotumika nchini?

Serikali inadhibiti vipi maduka ya vifaa vya magari vilivyotumika nchini?

Redpanther

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
2,823
Reaction score
3,816
Habari za wakati huu tena Dada na Kaka zangu, ni jioni nyingine tena ya siku ya Jumapili ya tarehe 20/06/2021 ambayo mimi Binafsi ni mzima Afya natumaini pia hata nyinyi mko salama.
Acha niende kwenye maada moja kwa moja..! Kuna wizi wa vifaa vya magari na magari yenyewe umeshamiri sana Hapa mjini na sehemu zingine. Vifaa ambavyo mara nyingi sana huibiwa ni Betri za Magari na vingine vingi tu. Kitu cha kujiuliza hapa chap chap, ni wapi hivi vifaa huuzwa ? Kwa watumiaji wa magari au Wauzaji wa vifaa vilivyotumika vya magari ambayo hii inaweza kuwa na 90% ya soko la vifaa hivyo.
Je Mamlaka zinazohusiana na usalama wa Raia na Mali zao zina shughulika vipi na hili suala la uuzaji wa vifaa used vya magari kwenye maduka ambalo ndio soko kubwa la bifaa vilivyoibiwa ??
Nina picha na video za watu wameibiwa gari na kuikuta imesambartishwa wamebakiza plate number na body tu mengine waneondoa..! Huku nikurudishana nyuma kimaendeleo
aa92ebc9-7dca-4db0-83af-41c620f09ca7.jpg

c666a97a-e57b-45e3-959b-b356ce125f67.jpg

da3a1dc3-cc97-4ecf-bd5d-25bbd934c015.jpg

608bd243-e4f2-45b3-8090-96b3f10f45ca.jpg

760a3240-cdfd-4c00-9b83-3b5072d7f6dd.jpg

TUKIACHANA NA HIZI PICHA; KUNA VIDEO AMBAYO VIBAKA WAMEINGIA KWA KWA MTU KURUKA GETI NA KUWAUA MBWA WANAOLINDA PALE NA KUIBA ESSENTIALS ZA GARI..! VIDEO IMZEINGUA KUPAKILIWA.
Ila kwa ufupi hii sihu serikali inashughulikia vipi ??
 
Daah aise inatia huruma ukute umejipiga piga.
Ndio maana watu wanaugua magonjwa ya ajabu ajabu time zingine kumbe pigo kama hizo.
 
Daah aise inatia huruma ukute umejipiga piga.
Ndio maana watu wanaugua magonjwa ya ajabu ajabu time zingine kumbe pigo kama hizo.

Sure Mzee! Unaweza ukaugua ugonjwa ambao haujawahi kuwahi kuwepo na ukafa ghafla. Umejichanga changa pesa mara paaap..! Gari imeibiwa
 
Serikali inapaswa ibadili namna ya kushughulikia jambo kama hili inaumiza sana , Tumefikia huku ??? Namna ya kutoa vibali kwa wamiliki wa maduka , lkn pia ...ikiwezekan iandaliwe mitego wanaofanya michezo hiii mbn ni rahisi kuwakamata , iwe kama kampeni ya kutokomeza ....biashara ya madawa ya kulevya Tz bila madawa inawezekana kwa nn. Ishindikane kwa hizi spare part za magendo ?????... Huuu ni mdao na kuna wafanya biashara wakubwa wanafadhili ndio maana soko lipo la kutosha

sent from HUAWEI
 
Umenena vyema Mkuu, kuna haja ya kuwepo kwa udhibiti na utoaji vibali kwa dealers wa used spare parts. Hii kitu isikie kwa mwenzako tu, unaumiza sana.
 
Ukiona jambo fulani serikali limekalia kimya ujue kuna mkubwa anafaidika nalo.
 
Watu ni wakatili sana aisee daah, aliechora huu mchoro itakua ni fundi roho imeniuma kama vile gari ni langu..tena haina muda maana ni registration ya Jan-April 2020
 
Watu ni wakatili sana aisee daah, aliechora huu mchoro itakua ni fundi roho imeniuma kama vile gari ni langu..tena haina muda maana ni registration ya Jan-April 2020

Eeeh mzee. Huo mchongo umechorwa sijui kuanzia Car wash ? Wakauweka vizuri wakachonga na ufunguo bandia.
 
Back
Top Bottom