Serikali Inaendelea na Utekelezaji Miradi ya Kusambaza Umeme - Ngorongoro

Serikali Inaendelea na Utekelezaji Miradi ya Kusambaza Umeme - Ngorongoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI INAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME- NGORONGORO

Na Godfrey Mwemezi, Ngorongoro Arusha.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji miradi ya kusambaza umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kuhakikisha kila Mwananchi anafikiwa na huduma hiyo .

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, ameyasema hayo leo, Mei 17, 2023 wakati wa tukio la kuwasha umeme katika nyumba ya Mjane Gladness Giloli, Mkazi wa Kijiji cha Sale, Wilayani Ngorongoro ,lililofanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Arusha.

Aidha, Naibu Waziri Byabato amewataka Wananchi wasioweza kumudumu gharama za wyring kutumia kifaa Maalum cha Ometa ili kuunganishiwa umeme kwenye nyumba zao kama alivyounganishiwa Mjane Gladness Giloli kwenye Makazi yake.

"Kila Mradi wa kusambaza umeme katika maeneo ya Vijijini unakuwa na Ometa takribani 250 ili kuwezesha wananchi wa kipato cha chini kumudumu gharama za kuunganishiwa umeme bila kutumia gharama kubwa"

Pia Naibu Waziri Byabato, amesema bei ya kuunganishiwa umeme kwa maeneo ya Vijijini ni shilingi 27000 tu lakini bei halisi ya kuunganishiwa umeme bila ruzuku iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita ni Shilingi 800,000 na hii ni kwa maeneo ya Mjini na Vijijini.

Hata hivyo, Byabato aliendelea kufafanua kuwa bei ya kuunganishiwa umeme katika maeneo ya Mjini kwa bei ya chini kabisa ni Shilingi 320,000 lakini bei halisi ni Shilingi 800,000 kama ingekuwa hakuna ruzuku iliyowekwa na Serikali.

Aidha mjane ,Gladness aliishukuru Serikali kwa kujali wajane kwani yeye ni mjane mwenye watoto watatu na kuongeza kuwa, umeme huo unamsaidia kujikwamua kiuchumi katika shughuli mbalimbali anazozifanya katika kujipatia kipato.

#WizaraYaNishati
#ByabatoKazini
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-18 at 14.24.57(1).mp4
    71.2 MB
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.44.jpeg
    74.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.49.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.49.jpeg
    71.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.47.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.47.jpeg
    88.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.46.jpeg
    57.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.45.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 14.02.45.jpeg
    77.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom