Serikali inafanya makosa makubwa kutumia Taasisi zake kujenga viwanda

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ni lazima tupongeze kwa dhati uamuzi wa serikali wa kujenga viwanda. ni maamuzi sahihi na tusipofanya maamuzi kama hayo tujue hakuna miujiza katika kupata maisha bora, maisha bora yanapatikana kwa kufanya maamuzi sahihi na kuyatekeleza kwa wakati.

Swali kuu hapa ni je serikali inatekeleza maamuzi haya kwa usahihi?

binafsi nina wasiwasi mkubwa kutokana na mambo yafuatayo.

kwanza ninajaribu kuangalia taasisi ambazo serikali inazitumia kujenga Viwanda, nikachukua Jeshi la magereza pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii. Ki msingi ukiangalia Jeshi la magereza wanayo miradi mingi kama ufugaji na utengenezaji wa thamani, kiwanda cha viatu na ujenzi wa majengo.

hivi ni mradi gani katika miradi yote iliyoko chini ya jeshi hili inaendeshwa kwa tija kibiashara? mathalani miradi ya ngombe unakuta mbali na kuwa na cheap labour lakini miaka nenda miaka rudi mifugo hii haiongezeki na hawafanyi biashara kusema wanauza kupata faida.

Sitaki kuzungumzia miradi ya kilimo, au ujenzi ambapo mbali na kuwa na wafanyakazi wa bure nyumba zao za kuishi tu wameshindwa kuzikarabati na kuziweka katika hali nzuri angalau kwa kufanya biashara kupata fedha za kununua vifaa na kutumia ufundi wa bure walionao kuweka nyumba za askari katika hali nzuri.

ninachotaka kusema ni kitu gani? hebu jiulize unaweza kumchukua mtu aliyezoea kutembea miguu peku ukamnunulia viatu siku moja na kumlazimisha kuvaa viatu? bila shaka atakuwa akikuona anavaa viatu na ukitoka anavua anatembea peku.

hivi unaweza kumchukua mtoto aliyezoea kwenda kwenye mziki mpaka usiku wa manane, hakuna shoo inayompita umfungie geti eti akae ndani? kimsingi mtoto huyu ataanza kujifunza mbinu mpya za kuruka fensi usiku na kutoroka kwenda kwenye mziki.

hebu watazame mifuko ya hifadhi ya jamii, hivi hawa wanafanya miradi gani yenye tija? kimsingi ni wataalamu wa kujenga majengo lakini ni nani amewahi kufanya tathmini ya gharama halisi inayotumika katika majengo haya kulinganisha na thamani halisi ya majengo yenyewe? tumeona ni mradi gani wa kibiashara wameufanya mifuko hii na wakauendesha kwa faida? sijui kama upo.

tunaweza kujiuliza hivi ni kwa nini huko nyuma tuliingia katika serikali kufanya biashara na tukashibdwa na wenzetu wenye kujua wakatushauri serikali ijitoe kwenye kufanya biashara na iwatengenezee mazingira sekita binafsi? sina uhakika kama tunajiona kuwa na ujuzi kuwashinda waliotushauri au tulielewa sababu zilizofanya watushauri hivyo.

nashindwa kuelewa kama tumeona tumepiga virungu viwili na tukajiamini kuwa tunaouwezo wa kuthibiti "corruption kiasi cha serikali kurudi kwenye biashra? ki msingi ni jambo gumu sana kwa serikali kujenga viwanda na kuviendesha.

1. ni kutokana na taasisi inazozitumia kuwa zimekwisha remaa. Yaani wamezoea kufanya miradi kwa hasara. kitaalamu wanasema ni bora mtu asiyejua anarekebishika lakini mtu anayejua jibu lisililo sahihi ni vigumu kufuta anachokijua na kumfahamisha kingine. Yaani hawa wamezoea mambo ya hovyo hivyo hata uawabane vipi watakachokifanya ni kujifunza mbinu za kiprofesional katika kufanya mambo ya hovyo. yaani kama unavyoona ukimfungia mtoto aliyezoea kwenda disco anaanza kujifunza kuruka ukuta na akaenda na kabla ya kucha akarudi akaruka ukuta hivyo kupiga virungu viwili tusijione tunaweza kudhibiti corruption hivyo tuzidi kuirundukia serikali biashara itaziendesha vizuri.

moja ya sababu ya serikali kujitoa katika biashara ni kudhibiti corruption hivyo mapambano yetu ya corruption yatakuwa na tija iwapo tutazidi kuielekeza serikali katika kujenga mazingira na kusimamia biashara tu.

2. Moja ya sababu kubwa zinazofanya taasisi za serikali kushindwa kufanya biashara ni watendaji wake kutokuwa na msukumo unaoleta ushindani kwenye biashara. mfano jambo linalosukuma makampuni kufanya vizuri katika biashara ni msukumo wa kutafuta faida unaotoka kwa wawekeza mitaji na kushuka chini hadi kwa wafanyakazi wenyewe. wawekezaji binafsi hawako tayari kupoteza mitaji hivyo kwa huweka usimamizi kuhakikisha mitaji yao inatumika vizuri lakini pia kutafuta motisha za kuwafanya wafanyakzi watimize wajibu wao. motisha hizi zinaweza kuwa adhabu kwa anayefanya vibaya na zawadi kwa anayefanya vizuri.

lakini kwa serikali kwanza wenye mitaji ambao ni wananchi wala hawana habari kama hiyo ni mitaji yao na pili wale wanaokabidhiwa dhamana huwa hawana machungu. matokeo yake hakuna taasisi ya umma inayojisikia vibaya kupoteza mtaji na badala yake hujali mlolongo wa maamuzi na mambo mengine yasiyo na tija ambayo mara nyingi ni chanzo cha upotevu wa mitaji.

kwa kifupi kama tunataka kujenga viwanda kama kujenga viwanda tunaweza kuzitumia taasisi za serikali kujenga viwanda lakini kama tunataka kujenga viwanda kwa kulenga faida. viwanda hivi viendeshwe kibiashara kwa maana vitusaidie kuagiza mashine na si bidhaa, vizalishe ajira kwa watanzania, vizuie fedha zetu kwenda nje kufuata bidhaa, tuzalishe bidhaa zivuke mipaka ziende nje kutuletea fedha za kigeni hatuwezi kuthubu kutumbukia katika kujenga viwanda kwa kutumia taasisi za umma na zenye uzoefu hasi katika kufanya biashra, bora kama wangekuwa na uzoefu sifuri.

nini serikali ingefanya.

serikali mitaji hii iitoe kwa watanzania katika sekita binafsi wazalishe wenyewe. huko nyuma tulikwama katika hili kutokana na corruption, tulivyoandaa mipango kama hii watendaji wa umma waliitumia kuhujumu, waliwapa watu wasio na sifa kwa kigezo cha undungu au rushwa.

tunapokuwa tumeinua rungu kudhibiti haya katika umma basi ni wakati wa mitaji hii tuiundie bank ya kuwakopesha wazalishaji kwa masharati nafuu.

tatizo kubwa la watanzania ni uwezo wa kupata mitaji lakini ujuzi wanao kwani hata hao wageni wanaofanikiwa wanawatumia watanzania hawa hawa. tutengeneze programu zinazowaleta watanzania wataalamu wenye fikra sawa wakopeshwe miundombinu na fedha ya kuanzia na serikai inaweza kumonitor account zao mpaka wanaporudisha mikopo ndio wanakuwa huru.
 
Tumeshashindwa tayari. Kujenga viwanda siyo sawa na ujenzi wa shule. Short and clear!
 
Maelezo mengi lakin ueleweki/ hayana content.
Wazo la hili kwangu ni zuri zaid kuliko taasis hiz kuendelea kujenga majumba makubwa ambayo input yake inachukua miaka mingi ni bora viwanda, kwanza itaeleta ajira kwa wengi na mzunguko wa pesa utaimalika na maisha ya watu yataboreka.
 


tatizo kubwa la watanzania ni kuzoea elimu za kukalili maswali na majibu na wewe ndugu yangu una tatizo hilo.

elimu hii ya kutosoma vitabu kutafuta maarifa inatufanya tunatoa majibu mafupi kwa hoja pana. usingekuwa mvivu wa kusoma ungejua changamoto iliyopo.

swali langu kwako mwalimu nyerere alijenga viwanda leo hii viwanda hivyo viko wapi vinatengeneza ajira gani?

ni kitu gani kilifanya viwanda vya mwalaimu nyerere vikafilisika mpaka tukaamua kuviuza.

leo walewale wanaonunua mita moja ya mraba kwa milioni 800 katika miradi wanayoitekeleza ndio hao tunawakabidhi viwanda.

tatizo ni elimu za kukalili maswali na majibu yaani ukijenga kiwanda unatengeneza ajira lakini maarifa ya katikati jinsi gani unatoka kwenye mtaji ukawa tranformed into bidhaa hatuhangaiki nao?
 
Tumeshashindwa tayari. Kujenga viwanda siyo sawa na ujenzi wa shule. Short and clear!


kuchagua kushindwa ni kuchagua umasikini wala hakuna nafuu katika hilo.

tumeamua kujenga viwanda ndio ni sahihi lakini utekelezaji tuwe makini ili tusiende kupoteza mitaji na tukaishia kuweka fedha za walipa kodi, tukashindwa kuviendesha na tukaviuza eti kuvibinafsisha.

inawezekana viongzi wanaona kujenga na vikafilisika tukauza kwa hasara ni biashara nzuri.
 
Mkuu kuwa mstaarabu kidogo.kwani ungeandika post ama comment yako bila kuandika NENO UELEWEKI ungekosa raha.Kiongozi kachambua mengi kwa mifano mizuri sana.Kikubwa kumtia moyo kwa uchambuzi wake... na wewe ungekuwa na chakuongezea basi ungeweka tu.
 
Tunahitaji kufikiri kujenga viwanda kibiashara na ndio hapo tutapata faida tunazozitegemea.

tujenge viwanda kwa gharama sahihi yaaani sio kuingiza mitaji ya kujenga viwanda viwili katika kiwanda kimoja.

tuzalishe na kufanya biashara ndio kodi za watanzania zinazowekezwa katika ujenzi zitazaa matunda.

hebu tazama makampuni binafsi ya simu na ttcl, hebu tazama shirika letu la ndege na mashirika binafsi, nk.

ki msingi ni vema serikali iondoe dhana ya kwamba kwa watanzania ama serikali yenyewe ijenge wakati dunia nzima imekwisha baini serikali kufanya biashara ni vigumu kuifanya kwa ushindani.

au waje wajenge wageni au watanzania waliokwisha kuwa tabaka la juu ndio wao waongezewe.

hatuwezi kuwazuia wageni kabisa lakii tuwakaribishe katika mambo madogo ambayo watanzania hawawezi kwa sasa na tusizibe mianya yote ili tuache nafasi za watanzania kukua na kuingia hukopia.

mambo ambayo watanzania wanaweza ila hawana mitaji basi wapewe mitaji kwa programu maalumu.

uko wapi mpango wa kuwasaidia watanzania wanaozalisha viatu kwenye vibanda vidogo mfano kuwakopesha mitaji ya kununua mashine ndogo ndogo na kuwapatia sori. wazalishe wakue na huko mbeleni miongoni mwao wapo watakaojenga viwanda
 
Mkuu ego kwa dhana halisi ya uchumi huria wa dunia ya leo upo sahihi kabisa. Kwa kuongezea tu nadhani kuna baadhi ya mambo serikali yetu sidhani kama kuna upembuzi yakinifu unakuwa umefanyika juu ya kwa nini viwanda vya umma vilikufa kwa wakati huo ambapo kulikuwa hakuna ushindani kama sasa.
Pili, serikali ilitakiwa itengeneze mazingira mazuri na bora yenye sera rafiki kwa wawekezaji kuanzia wa ndani wenye mitaji midogo hadi mikubwa na wawekezaji wa nje ambao watawekewa sera za kuwabana kuja kuwekeza katika biashara kubwa na sio biashara hizi za kusumbuana na Wachina Kariakoo hadi katika kuchoma mahindi
Serikali kama serikali ibaki katika nafasi yake ya kuhakikisha ukuaji wa sekta hii ili kuweza kukusanya kodi kubwa na sio kujiingiza katika biashara.
Ukija watendaji wengi wa serikalini si wafanyabiashara/wajasiriamali bali ni wanataaluma tu ambao kiuhalisia hawawezi kuendesha kiwanda au biashara ikawa na tija. Mathalani angalia mifano michache tu ya taasisi zake pamoja na kukusanya pesa lakini hazifikii malengo hivyo kushindwa kujiendesha na kupewa ruzuku na serikali.
 


ndugu yangu uko sahihi kabisa.

uchumi wa leo ni kila sekita kutambua wajibu wake ambao unaendana na maendeleo ambayo dunia leo hii imefikia.

si wakati wa ku "re intent the wheel", kwa kujaribu kufanya mambo ambayo dunia imekwisha baini ufanisi wake ni mdogo. ni wakati leo hii wa sisi kutambu8a sababu zinazofanya serikali zinajitoa katika kufanya biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…