Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SERIKALI INAFANYA TATHMINI YA UWEZEKANO WA KUPANGA BEI MOJA YA BIDHAA ZA PETROLI NCHI NZIMA
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema Serikali kupitia EWURA inafanya tathmini ya uwezekano wa kupanga bei moja ya bidhaa za petroli nchi nzima.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Aprili 3,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali namba 22 la Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuweka utaratibu ili bei ya mafuta ya Dizeli na Petroli iwe moja kwa nchi nzima.
Mhe. Kapinga amesema kuwa utaratibu huo ambao ulikuwa unatumika miaka ya nyuma ulikwama kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zilijitokeza kipindi hicho hivyo Serikali iliwaruhusu wafanyabiashara wa mafuta kupanga bei ya mafuta kulingana na soko