Serikali inakatisha tamaa wakulima kuendelea na kilimo, mazao yanaozea ndani kwa kukosa wanunuzi.

mjasiriamali mdogo

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
258
Reaction score
110
Watu tumeamua kujiajiri katika kilimo lakini cha kuskitisha hakuna soko la uwakika. Huku songea kipindi cha mavuno serikali ilinunua mahindi kilo kwa tsh 500 kwa muda mfupi ikatangaza kuishiwa fedha na magunia. Mbaya zaidi wakulima mpaka sasa tuna mahindi mengi sana na wanunuzi hakuna na wanaojitokeza kutoka nje ya nchi wanapata vikwazo kibao. Serikali tusaidie kututafutia soko la uwakika la mazao ili tuondolane na umaskin. Nawakaribisha wote mnaotaka kulima huku ardhi ipo kubwa na hakuna shida katika upatikanaji kwa kununua au kukodi. Karibu songea karibu ruvuma.
 
hawa viongozi hawana nia njema na wakulima kabisa.kulima ulime wewe tena kwa shida kweli na bei juu ya pembe jeo wao wanakuangalia tu kasheshe inaanza pale unapoanza mavuno,ndio wanaibuka mala oh kuna upungufu wa chakula nchini mipaka yote ifungwe!!!!wanaanza kuwaibia wakulima kwa kuwapa bei wanayotaka wao na hata hivyo hawayamalizi,wanaanza matamko tu huyu anasema hivi yule anaasema vile mi hiyo amri cjaipata!,waziri mkuu anasema mipaka iko wazi uzeni huko unakutana na watendaji wanasema hayo maagizo ni ya kisiasa c hatuyajui!!!bado mkulima una kuja kudanganywa tena na unacheka tu kama zuzu
 
Nchi haiendelei kwa kuwapokonya wenye nacho, bali kuhakikisha kila mwananchi analipa kodi. Pia kodi inayolipwa lazima iwanufaishe wananchi wote. Kuwapokonya wenye nacho na kuwapa wasio nacho ni kurudi nyuma kwani wapo wasionacho kwa sababu hawana uwezo wa kumiliki. Ukiwapa utajikuta wametapanya na wanarudi kwenye hali yao ya zamani. Serikali lazimi ielewi hili ili mimi ninapolima isifikiri kwamba nia yangu ni kuwasaidia masikini tu bila faida.
 
Ninaamini kama itafika siku wakulima wakawa na Vyama halisi kabisa vya Ushirika vilivyoundwa na kuendeshwa kwa maslahi hasa ya Wakulima, tutapata suluhisho la unyanyasaji huu kwa Wakulima. Ninaongelea Vyama Vya Ushirika vya Wakulima sio hivi vya Kisiasa vilivyopo. Kwa Wakulima wa Ufuta huko Rukwa, Wakulima wa Alizeti huko Singida, Wakulima wa Mpunga huko Morogoro, Mbeya na kwingineko wakaunda Vyama vyenye uwezo wa kufikisha Serikali Mahakamani ili kutetea maslahi ya Wakulima. Ninajua kuna Wataalamu wa masuala ya Vyama vya Ushirika, wapo. Wanaweza kunielewesha kama hilo linawezekana. Inatia machungu sana!!
 
Serikali ingefanya jitihada za kufufua mashine za MNC zilizopo Iringa, Dar na Arusha ili iuze unga badala ya mahindi.Fedha nyingi na ajira zinapotea kwa kuwaacha wakulima wahangaike na masoko wakati ni kazi ya vyama vya ushirika na serikali.
 
Watu tumeamua kujiajiri katika kilimo lakini cha kuskitisha hakuna soko la uwakika. Huku songea kipindi cha mavuno serikali ilinunua mahindi kilo kwa tsh 500 kwa muda mfupi ikatangaza kuishiwa fedha na magunia. Mbaya zaidi wakulima mpaka sasa tuna mahindi mengi sana na wanunuzi hakuna na wanaojitokeza kutoka nje ya nchi wanapata vikwazo kibao. Serikali tusaidie kututafutia soko la uwakika la mazao ili tuondolane na umaskin. Nawakaribisha wote mnaotaka kulima huku ardhi ipo kubwa na hakuna shida katika upatikanaji kwa kununua au kukodi. Karibu songea karibu ruvuma.

pole sana. asante kwa kutukaribisha kulima ruvuma. huko ardhi/shamba linapatikana kw kiasi gani kwa hekari?
 
Watu tumeamua kujiajiri katika kilimo lakini cha kuskitisha hakuna soko la uwakika. Huku songea kipindi cha mavuno serikali ilinunua mahindi kilo kwa tsh 500 kwa muda mfupi ikatangaza kuishiwa fedha na magunia. Mbaya zaidi wakulima mpaka sasa tuna mahindi mengi sana na wanunuzi hakuna na wanaojitokeza kutoka nje ya nchi wanapata vikwazo kibao. Serikali tusaidie kututafutia soko la uwakika la mazao ili tuondolane na umaskin. Nawakaribisha wote mnaotaka kulima huku ardhi ipo kubwa na hakuna shida katika upatikanaji kwa kununua au kukodi. Karibu songea karibu ruvuma.

Pole mzee nipo huko tang mwez march 2013 nimeon hali halis na has gharm za uzalishaj!
 
Mada ni nzuri, watanzania tuache mambo ya assumption kuzingizia Mungu na hekima, tunahitaji viongozi wenye mtazamo chanya na kizazi kijacho, wengi wao wa sasa wanajitazama wao na familia zao tu,mtu ana mabilioni ya pesa lakini msosi wa elfu tatu hamalizi! Ni ubinafsi mtupu sasa tunataka katiba inayoweka wazi uwajibikaji na uwajibishwaji wa kila kiongozi na raia,asante.
 
Watu tumeamua kujiajiri katika kilimo lakini cha kuskitisha hakuna soko la uwakika. Huku songea kipindi cha mavuno serikali ilinunua mahindi kilo kwa tsh 500 kwa muda mfupi ikatangaza kuishiwa fedha na magunia. Mbaya zaidi wakulima mpaka sasa tuna mahindi mengi sana na wanunuzi hakuna na wanaojitokeza kutoka nje ya nchi wanapata vikwazo kibao. Serikali tusaidie kututafutia soko la uwakika la mazao ili tuondolane na umaskin. Nawakaribisha wote mnaotaka kulima huku ardhi ipo kubwa na hakuna shida katika upatikanaji kwa kununua au kukodi. Karibu songea karibu ruvuma.

Pole sana mkuu wakati wewe unalia na soko la mahindi sisi huku Morogoro tumalia na soko la Munga wakati tunaanza kuvuna mpunga mwakajana serikali hii inayojiita sikivu ilizuia mchele usivuke mipaka ya nchi na ikaruhusu vigogo serikalini waingize mchele toka nje matokeo yake mpaka leo hii mashine zote za kukoboa mpunga zimejaa na watu wamekosa hata sehemu ya kuhifadhi mpunga na sasa mpunga unanyeshewa mvua kisa hakuna soko kabisa na msimu wa kulima umefika watu hatuna la kufanya ila tumepanga kuwajibu mwaka 2015 kwenye masanduku ya kura kwanini serikali hii isiache soko huria mkulima auze mazao yake popote duniani anapo ona pana maslahi kwake? Uonezi huu mwisho 2015
 
Back
Top Bottom