Serikali inakopa kwa 16% wakati wenzetu wanakopa kwa 2%-3%!!!!

Serikali inakopa kwa 16% wakati wenzetu wanakopa kwa 2%-3%!!!!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Serikali ya Tanzania haina ubunifu kwa sasa wanachukua mikopo kwenye bank zetu na mashikika ya kijamii kama NSSF kwa 16% wakati serikali nyingine duniani zinakopa kwa 2%-3%. Kitendo cha serikali kuchukua mikopo kwa riba ya juu vilevile kinasababisha mikopo ya bank kuwa juu hasa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Hizi riba za juu kwa biashara za kati na ndogo inasababisha hizi biashara kushidwa kukuza biashara na hii inasababisha kutokuajiri. Hivyo kama unataka kujua kwanini ajiri ni chache sababu mojawapo ni serikali kuchukua mikopo bank kwa riba ya juu sana. Seruikali inatakiwa kutafuta pesa kwa wawekezaji nje na kwenye mabank ya kimataifa na kuachia pesa za ndani zikopwe na biashara ndogo ndogo ambazo ndizo zinatoa ajira kwa riba ya chini. Ni vigumu kukuza biahsra kwa riba za 20%-25% na vilevile kuajiri watu. Huko nchi za Ulaya kuna serikali zinazokopa kwa 1% tu!!!. Sasa serikali na bank kuu wanatakiwa kuwa wabunifu badala ya kutoa sababu kila siku wakati sababu ni serikali.
 
Back
Top Bottom