Mimi wasiwasi mkubwa ni kuwa hii mitaihani ipo chini ya mkaguzi mkuu wa Elimu Kanda, na hawa huwa wanashindana ni yupi kafaulisha sana ni yupi kafelisha sana hivyo itakuwa ni rahisi sana kwao kuanza kuchakachua matokeo kwani kila mmoja hatotaka kuwa nyuma ya mwenzake.
Hivyo nitoe ushauri wangu wa dhati wa Waziri mwenye dhamana na elimu ndani ya Nchi, kuwa kama kweli ana nia njema na Taifa hili hii mitihani airudishe kwenye chombo amabacho mimi kama mimi nina imani nacho sana kiitwacho Baraza la Mitihani la Taifa a.k.a NECTA, hapo ndipo suluhu ya elimu itafahamika ndani ya Taifa letuuuu!!!