Serikali inapaswa kuigawa tena Wilaya ya Kilosa kutokana na ukubwa wake

Serikali inapaswa kuigawa tena Wilaya ya Kilosa kutokana na ukubwa wake

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Miongoni mwa wilaya zenye idadi kubwa ya kata hapa nchini Tanzania ni wilaya ya kilosa. Wilaya ya Kilosa ina jumla ya kata 38 mara baada ya kugawanywa kidogo na kuzaa wilaya ya gairo yenye kata 8.

Kata za Wilaya ya Kilosa - Mkoa wa Morogoro - Tanzania ni

Berega | Chanzuru | Dumila | Kasiki | Kidete | Kidodi | Kilangali | Kimamba A | Kimamba B | Kisanga | Kitete | Lumbiji | Lumuma | Mabula | Mabwerebwere | Madoto | Magole | Magomeni | Magubike | Maguha | Malolo | Mamboya | Masanze | Mbigiri | Mbumi | Mhenda | Mikumi | Mkwatani | Msowero | Mtumbatu | Mvumi | Parakuyo | Ruaha | Rudewa | Ruhembe | Tindiga | Ulaya | Uleling`ombe | Vidunda | Zombo |

Wilaya ya kilosa eneo linalokadiriwa kuwa kilometa za mraba 11773 ikiwa ni zaidi ya mara 8 ya ukubwa wa eneo la mkoa wa Dar-es-Salaam.

Kiuendeshaji na kiutawala ni ngumu sana kwa wilaya kama hii kupata maendeleo ya haraka kutokana na ukubwa wa eneo lake.

Wito wangu kwa serikali ni kuwa iigawe tena hii wilaya katika wilaya nyingine 2 ...Ipatikane Wilaya ya Dumila na wilaya ya Mikumi. Ili kurahisisha masuala mazima ya kiutawala na maendeleo kwa ujumla.

Ni hayo tu.
 
Uzi tayari
Ungeweka na ramani..ilivyo sasa na itakavyokuwa baada ya kuigawa.

Pia, kwenye maelezo yako weka baada ya kuigawa itabaki na kata ngapi na zipi? na zile kata za wilaya nyingine.

Hii pia inaweza kusaidia kwenye ile hoja ya kuugawa Mkoa wa Morogoro.
 
Mwenye kuifahamu Wilaya ya Mufindi naomba aje anipe ukubwa wake. Maana na kwenyewe siyo haba. Na ile miundombinu yake mingi ya barabara ilivyo duni!! Ni shida juu ya shida.
 
thumb_112_370x300_0_0_crop.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Miongoni mwa wilaya zenye idadi kubwa ya kata hapa nchini Tanzania ni wilaya ya kilosa. Wilaya ya Kilosa ina jumla ya kata 38 mara baada ya kugawanywa kidogo na kuzaa wilaya ya gairo yenye kata 8...
Ikikubalika hiyo wilaya iitwe Mabwerebwere
 
Back
Top Bottom