Serikali inapaswa kuliangalia hili suala la kamali(BETING)

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Nimestuka kidogo nilipokwenda kibaha kutembea kwa ndugu yangu, kitu ambacho kimenishangaza kumezagaa vimashine vya kucheza kamali sijapata ona.
Yaaan kila kwenye frem tatu lazima kiwepo, harafu hakina usimamiz maalum, yaaan watot wanacheza nje nje kwa mtaji wa shilling 200/=. Serikali angalieni hili jambo jamani, watoto hawasomi kabisa
 
Viwanda hivyo

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji16]
 
Hili suala lisipodhibitiwa basi madhara yake yatakuwa makubwa mno.

Fikiria hiki kizazi kinachokuwa kizazi cha wanafunzi kuanzia primary hadi secondary kinachojiingiza kwenye haya makamari.

Baada ya miaka kumi mbele tutakuwa na kizazi cha aina gani??

Kizazi kisichofikiri kwenye kufanya kazi,nguvu kazi inapotea bure kwa vijana kushinda kwenye mabanda ya kamari bila kuzalisha kitu chochote.
Na tazama baada ya kuona soko la uhakika angalia makampuni ya kamari yalivyoshika hatamu kipindi hiki na yataongezeka zaidi na zaidi.
Unaona hadi viongozi wa serikali wanashiriki kupromote biashara hii kwa kuwakabidhi washindi hundi zao na zawadi mbalimbali.

Wenzetu kamari ni hobby huku kwetu tunataka kugeuza kazi.

Serikali chukueni hili suala kwa umakini mkubwa,kizazi kinakwenda kuangamia,tusisubiri hadi tuangamie ndio tupige marufuku.

Hapa tuamue kati ya kodi(revenue gainsVS society welfare)

Uamuzi ni wetu...!!tuchukue hatua
 
Hayo ni mambo ya kupita tu huu ni wakati wake so itafika muda yataisha thamani. Mfano mzuri miaka ya 2000 lilikuja wimbi kubwa la mabanda ya video.., yakapita likaja vibanda vya play station nayo yakapita. Kwa sasa ni hayo madubuwasha muda wake ukiisha nayo yatapita, ni moja ya stage katika maisha na ukuaji wa mtoto.
Binafsi siwezi umiza kichwa kwenye mambo ya mpito
 
Ni hatari kupita kiasi. Madenti kibao hawaendi shule wanashinda ku bet

Hili dude halina uangalizi kbs wa umri mpk watoto wadogo wanacheza masaa yote...Gaming board inabidi wakataze hili dude halifai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…