maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Hakuna biashara inayonishangaza kama biashara ya mabondo ya sangara, mabondo ambayo bila shaka yako kwenye orodha ya nyara za serikali lakini isiyojaliwa na serikali.
Biashara hii ambayo imefanywa katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa zaidi ya miaka 20 hivi sasa na wahusika wake wakubwa wakiwa ni wachina haionyeshi kama imerasmishwa ama inaingiza kodi yoyote serikalini.
Ebu fikiria kilo moja ya mabondo ya sangara inanunuliwa na wachina kati ya shs 150,000 na 400,000 kutegemea na saizi ya bondo lenyewe wakati huo huo kilo ya sangara ni kati ya shs 4000 na 20000 kutegemea na ukubwa wa samaki lakini pesa hiyo yote haina risiti na haikatwi kodi.
Swali ninaloiuliza serikali ni kama inaijua biashara hii ya mabondo ambayo hata ufanywaji wake hauna risiti, vibali, leseni wala kukatwa kodi.