Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Wanaoleta maendeleo haswa ni wananchi walipa kodi wakisimamiwa na watumishi wa umma. Viongozi wa serikali wao kazi yao kutunga sera tu.
Tumeona mara nyingi serikalini inapojisifu kupiga hatua kiuchumi sifa zote anapewa Rais aliyeko madarakani na wanaompa hizo sifa haswa ni wale viongozi wa kuteuliwa ili kulinda unga wao.
Watumishi kwa makusudi kabisa wanasahaulika katika hayo maendeleo aliyofanya Rais mtukufu. Zaidi utasikia kauli za boresheni utendaji wenu, ongezeni juhudi na ubunifu ili uzalishaji uongezeke ndipo mishahara iongngezwe.
Kauli nyingine ya kipuuzi ni ile tumedhibiti mfumuko wa bei kuliko kuongeza mishahara, mbona mishahara yao hawaishushi kama fedha ndogo unaweza kufanya jambo kubwa?
Mei Mosi njema.