Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Tuseme unayoyasema ni kweli. Jee Serikali haiwezi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuweka akiba?Bajeti ya Tanzania ni tegemezi kwa asilimia kubwa, kwa muktadha huo si rahisi kuweka akiba ya kutosha ya pesa. Labda kama wameanza kuweka akiba ya dhahabu kama malighafi.
Ripoti ya CAG inaonyesha ubadhirifu na matumizi yasiyoeleweka ya zaidi ya shilingi Trillion 1. 5 katika mwaka wa fedha unaoisha Julai. Ambapo zaidi ya shilingi bilioni 600 ni mashirika ya umma, serikali kuu bilioni 300, serikali za mitaa na halmashauri ni bilioni 130. Kama uwajibikaji hakuna katika matumizi ni wazi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ni jambo lisilowezekana.Tuseme unayoyasema ni kweli. Jee Serikali haiwezi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuweka akiba?
Na nadhani watawala wetu wamejua watanzania wanadhani maendeleo huletwa na watu binafsi nje ya mipango ya Serikali.Sidhani hata kama kwenye kamusi ya serikali kuna neno AKIBA
Nchi zingine wanaweka sana dhahabu
Sisi tunajua madeni tu na sidhani hata kama yatakuja kwisha
Halafu wengi wanajua deni la Taifa ni kiasi gani, ila hawajui kuwa tunalipa Riba tu deni linaongezeka kila kukicha
Wengi hawajui haki zao kabisa na hata serikali ni niniNa nadhani watawala wetu wamejua watanzania wanadhani maendeleo huletwa na watu binafsi nje ya mipango ya Serikali.
Kwa watanzania wengi Serikali ni dubwasha fulani hivi lisilo na mahusiano nao kwa maisha yao ya kila siku kiuchumi!