Serikali inapoteza mapato huku

Serikali inapoteza mapato huku

Lihove2

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2018
Posts
3,545
Reaction score
6,512
Kwa udhibiti huu wa Internet, mapato kwa makampuni ya simu yatashuka sana, hivyo kiasi cha kodi kushuka pia. Kwa sasa mobile companies wanauza sana data kuliko voice. So kwa kuwa siku hizi huwezi download chochote, wala huwezi angalia Online TV, pamoja na movies bundle halitumiki isipokuwa mpaka hayo ma-VPN sijui

Kimsingi watanzania wanasave, ila pia mapato ya Serikali yatapungua pia kwa sababu mauzo ya bundles yatashuka.

Nadhani kuna wanaoanza kuangalia uwezekano wa kulipia hizo VPN, hivyo mapato yatakwenda nje ya Nchi.

Naomba muendelee nilipoishia.
 
Kampuni za simu zimepata hasara kubwa na VPN kapata faida kubwa mno , wanaombea internet iendelee kuzorota waendelee kupiga pesa bila kelele
Na makampuni ya simu hayatokili wazi kuwa yamepata hasara.
 
Kama unajidanganya wanapata hasara bas tambua huwez jiunga hyo vpn yako bila kua na bando la internet... So hakijaaribika kitu
 
Kampuni za simu zimepata hasara kubwa na VPN kapata faida kubwa mno , wanaombea internet iendelee kuzorota waendelee kupiga pesa bila kelele
Hamna point za msingi zaidi ya kulalama kwa kila jambo. Kuna ubaya gani usalama wa nchi ukilindwa? Mapato yapo tu ndio maana tunaanza kujenga uwanja wa michezo Dodoma. Au mnataka mpewe Chadema mjenge ofisi?
 
Hamna point za msingi zaidi ya kulalama kwa kila jambo. Kuna ubaya gani usalama wa nchi ukilindwa? Mapato yapo tu ndio maana tunaanza kujenga uwanja wa michezo Dodoma. Au mnataka mpewe Chadema mjenge ofisi?
labda usalama wa ccm siyo wa nchi

Hapo mnawapa tu akili watanzania waamini kumbe intaneti ina nguvu kuliko chochote na siku nyingine wataitumia hiyo hiyo intaneti kufanya yao

Kwa kawaida maandamano ya kupata uhuru au ya kuvunja ujinga kama huu wa kuzimiana intaneti huwa hayapangwi wala kuratibiwa wala hayahitaji intaneti bali utaona tu kimenuka
 
asilimia 1 tu ya raia wa Tanzania ndiyo wanajuwa kutumia vpn, asilimia 99 hawajuwi vpn ni nini na inatumiakaje na inapatikana wapi

kwahiyo hasara ipo pale pale
Sababu wataona hamna sababu yakununua vifurushi vya internet na kuamua kuwa wananunua dk na sms pekee...Hasara haiwakwepi.
 
Nilikuwa nalipia bundle Smile la Tshs 34,500 , 10 GB, kwa mwezi.
Kwa mwaka karibia 414,000( au $178).
WAMEZIMA!

NIKAINGIA VPN.
Nimelipia KWA MWAKA $49.9!

Nawapongeza TCRA kwa kutufungua macho.
Waendelee kufunga data mitandao.
+ Bundle la internet kutoka kwa ISP wako...Au vpn unayotumia wewe wanakupa na package ya data?
 
Back
Top Bottom