Serikali inapuuza Ripoti za CAG au inawalinda wezi?

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Jamani ukifatilia ripoti za CAG pamoja na kuweka wazi wahusika wa upotevu mkubwa wa fedha za Umma lakini Serikali imekuwa haichukui hatua kali dhidi yao na ndio sababu matukio ya upigaji yanajirudia

Mara zote CAG na Bunge wamependekeza hatua za kuchukua lakini Serikali haiwawajibishi wanaotajwa kuhujumu fedha huku ikiendelea kuwaumiza wananchi kwa Kodi zisizoeleweka kila wakati

Sasa kuna umuhimu gani Serikali kutangaza taarifa za ubadhirifu bila kuwaadhibu wanaofisadi Miradi na Fedha za Walipa Kodi? Je, Serikali ina uhusiano nao na inawatuma?

Kwa nini Serikali haitoi Adhabu kali kwa wanaohujumu Fedha za Umma kwenye Ripoti za CAG? Je, inahusika na ubadhirifu huo?
 
Tumbili hupambana na mwenzake tu endapo amezidiwa katika ukwapuaji wa ndizi mbivu !!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Serikali ni ya sisiem
Bunge ni la sisiem
Mahakama ni ya sisiem
Sasa ni nani atamgusa nani?
 
Back
Top Bottom