Serikali inataka Mo asifunge viwanda vyake vya chai vilivyokufa, mantiki iko wapi?

Serikali inataka Mo asifunge viwanda vyake vya chai vilivyokufa, mantiki iko wapi?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kuna mambo yananishangaza sana kuhusu serikali ya Tanzania.

Hili la serikali kumzua Mo asifunge viwanda vyake vya chai vilivyojifia limenishangaza sana. Bado sijapata mantiki kabisa.

Kama lengo ni kuwalinda wakulima wa chai, kwanini serikali kwa miaka yoyote imeshindwa kujenga viwanda vya chai na kuwafanya wale wakulima kuwa wabia katika umiliki na uendeshaji wa hivyo viwanda?

Viwanda vile ni mali ya Mo, hana ubia wowote na serikali, na kwa muda mrefu amekuwa akiviendesha kwa hasara kubwa isiyoweza kuepuka kwa 100%, hivyo suluhisho likawa ni bora avifunge ili maisha mengine yaendelee.

Kama serikali inaona vile viwanda ni mali sana kwanini asivinunue ili iviendeshe yenyewe?

Fursa/adhabu hii ya serikali kuzuia kufungwa kwa viwanda kwanini iwe kwa Mo tu?

Kumzuia mfanyabiashara asifunge biashara yake kuna athari hizi;

1. Ni kuvunja katiba kwa kuingilia uhuru wa mmiliki.

2. Kunaongeza mzigo wa gharama kwa mmiliki pasipo sababu.

3. Kunatengeneza harufu ya rushwa, ufisadi, upendeleo na skendo kwa serikali ikiwa serikali itagharamia fidia ya hasara ya mmiliki kuendelea kuendesha hivyo viwanda.

Mwisho kabisa, hisia zangu zinanituma kuona huu ni mchezo wa Mo na wanasiasa kuvuna pesa za serikali kifisadi, kwa sababu kwa sehemu kubwa vile viwanda vilikuwa taabani kujifia, kwa muda mrefu havitengenezi faida na huenda visitengeneze faida kamwe.
 
Back
Top Bottom