Serikali Inatambua Umuhimu wa Kukuza Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake - Majaliwa

Serikali Inatambua Umuhimu wa Kukuza Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake - Majaliwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

GlWqQQCXAAADeuE.jpg

Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo Machi 6, 2025 amezungumza na wanawake katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi.

Mgeni Rasmi wa Kongamano la Siku ya wanawake Duniani kanda ya Kusini Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowasili viwanja vya maegesho wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi alipokewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telacky , kwa ajili ya kongamano hilo.

GlWLiI-XgAAwt-U.jpg


Akifungua kongamano hilo, Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi na kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wanawake kuendelea kuhamasishana na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo mikopo inayotokana na halmashauri (10%) na taasisi za kibenki kwa kuzingatia mikopo yenye masharti nafuu ili kutoathiri maendeleo na mienendo ya maendeleo ya mwanamke na mjasiriamali.

Screenshot 2025-03-06 at 21-18-53 Instagram.png


Kupitia kongamano hilo lililowakutanisha wanawake kutoka Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, wanawake wametakiwa kuanzisha viwanda vidogovidogo vya uchakataji ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo wanayoyazalisha ili kujiongezea kipato kupitia kuuza bidhaa badala ya malighafi.

Viongozi mbalimbali kutoka Wiliya na Mikoa ya kanda ya kusini wamehudhuria katika kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi leo Machi 6, 2025 .

Kauli Mbiu ya Kongamano hilo kwa kanda ya kusini ni: "Ushiriki na Mchango wa Wanawake katika kukuza Maadili, Uzalishaji na Kuongeza Mnyororo wa Thamani ya Mazao"
 

Attachments

  • GlWKjaRWgAEnv8R.jpg
    GlWKjaRWgAEnv8R.jpg
    549.7 KB · Views: 1
  • GlWKjaRXgAAMMyG.jpg
    GlWKjaRXgAAMMyG.jpg
    504.3 KB · Views: 1
  • Screenshot 2025-03-06 at 21-18-35 Instagram.png
    Screenshot 2025-03-06 at 21-18-35 Instagram.png
    1 MB · Views: 1
  • Screenshot 2025-03-06 at 21-19-22 Instagram.png
    Screenshot 2025-03-06 at 21-19-22 Instagram.png
    811.1 KB · Views: 1
  • GlWqQQDWYAATqma.jpg
    GlWqQQDWYAATqma.jpg
    268.7 KB · Views: 1
  • GlWqQQJXMAAAk71.jpg
    GlWqQQJXMAAAk71.jpg
    372.9 KB · Views: 1
  • GlWqQQIXwAEmv6o.jpg
    GlWqQQIXwAEmv6o.jpg
    450.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom