kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Rais Samia Suluhu amemaliza Ziara yake leo mkoani Manyara kwa kukagua Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara. Baada ya ukaguzi huo alikutana na kuzungumza na wananchi. Kabla ya Rais Samia kuzungumza. Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alipata nafasi ya kuzungumza na kuongelea jinsi Serikali ilivyojipanga kuzalisha ajira kupitia kilimo na kupunguza tatizo la ajira nchini.
Serikali imeanzisha mashamba ya pamoja zaidi ya hekari 188,000 ambazo zitagaiwa na kumilikishwa kwa vijana. Aidha mradi huo utagharimu Shs. Bilioni 200 na kutengeneza ajira 40,000 ndani ya miaka 3. Pamoja na hayo Serikali imeongeza bajeti ya kilimo ili kujenga mabwawa ya umwagiliaji yatakayosaidia kuachana na kilimo cha kutegemea mvua.
"Hukutaka kuwalaumu vijana kwa kutokufanya kazi uliamua kuweka fedha ili vijana wa kitanzania kuingia mashambani"-Mhe. Waziri Hussein Bashe