Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo kwa sasa imekumbwa na Wingi wa vijana ambao hawana Ajira hii inatokea kwa sababu ajira zilizopo ni chache na wasomi wanao tegemea ajira wao wakiwa wengi. Hivyo tatizo la ukosefu wa ajira ndipo linapo chipukizi.
Sababu zinazo fanya kuwepo na vijana wengi wanao tegemea Ajira
1- Serikali haiwapi vipaumbele vijana wanao somea Taaluma za ufundi.
Hapa serikali inaonyesha kutokua na vipaumbele kwa vijana wanao soma baadhi ya taaluma kwa mfano Tanzania ni rahisi kutoa mikopo kwa Asilimia kubwa kwa wanao soma ualimu na kuwapa mkopo wa asilimia ndogo kwa wanafunzi wanao somea ufundi.
Hapa bila shaka bila shaka vijana wengi watakimbilia kusomea ualimu ili wapate mkopo na kuacha kusomea taaluma ya ufundi kwa kuogopa kukosa mkopo hivyo wengi watakimbilia kusomea ualimu na huko ndo kutakuwa na vijana wengi hivyo ajira inaweza kua changamoto.
Hivyo serikali inapaswa kuwasamini wanafunzi wanao chagua ufundi kwa maana wao hawata kua tegemezi kwa ajira serikalini bali wanauwezo wa kwenda kujiajiri katika Taaluma husika mwanafunzi aliyo soma.
2- Serikali kuthamini elimu ya makaratasi zaidi ya elimu ya vitendo
Hii inaibua changamoto nyingine kubwa kwa Tanzania yetu elimu ya makaratasi inaweza kua imepewa kipaumbele zaidi ya elimu ya vitendo.
Ukilinganisha elimu ya nchi zilizo endelea na elimu ya nchi yetu basi kutakuwa na utofauti mkubwa sana kwa sababu wasomi wengi wa Tanzania hutembea na bahasha zenye makaratasi na vyeti mbalimbali kuliko kutembea na taaluma zao. Hivyo hapa kuna utofauti mkubwa sana zaidi ya nchi za wenzetu ambao wao pengine wamejikita kwenye elimu ya vitendo mfano wamejizatiti kukuza technologia hivyo ndio maana wao elimu yao inaonekana kua bora zaidi ya elimu yetu. Hapa tunapaswa kama taifa kubadili mfumo na kuwafanya vijana kupenda ufundi zaidi ya taaluma nyingine.
3- Kutopewa vipaumbele Vijana Wenye vipaji
Bila shaka kuna vijana wengi wenye vipaji hapa hapa Tanzania na Endapo vipaji vyao vitafanyiwa kazi haitatokea wao kua tegemezi wa ajira.
Tanzania ni moja ya nchi ambayo ipo nyuma kwenye kuwasaidia vijana wenye vipaji yaani wanathamini vijana walio soma elimu ambayo pengine haina msaada zaidi ya wale wenye vipaji. Kwa mfano imetokea vijana kuvumbua vitu lakini mwisho wao hauna matunda kwa sababu ya kuwepo sheria kandamizi na kutokuwepo na msaada kwa vijana hao hivyo mtu hawezi kujikita kufanya ubunifu wakati anajua pengi6ataishia pabaya hivyo itamubidi afuate kile ambacho serikali inaonekana kukipa kipaumbele.
Serikali inatakiwa kuwapa vijana wabunifu na wenye vipaji msaada ili kufikia malengo yao endana serikali itafanya hivyo basi itapunguza ombwe la vijana kukosa ajira.
4- Uchaguzi wa wanafunzi vyuoni
Licha ya serikali kujua kua kuna upungufu wa ajira kwenye sekta fulani lakini bado serikali inawasukuma vijana kwenda kusoma taaluma hizo.
Kwa mfano serikali inajua kwamba hakuna ajira za ualimu lakini licha ya hilo serikali bado inapeleka vyuoni vijana wengi kusomea ualimu wakati hakuna ajira.
Ni kazi kubwa sana kumwambia mwanafunzi aliye soma ualimu kwenda kujiajiri. Kwa mfano kijana amesoma ualimu wa somo la kiswahili, je ataenda kujiajiri wapi? Hapo hapo mbaya zaidi mwalimu huyo akiamua ajira kua walau mtunzi wa vitabu mwisho wake atakutana na tozo kandamizi ambazo zimewekwa hivyo kumfanya abaki kutegemea ajira tu.
Pia kuna sababu nyingi sana ambazo zinafanya vijana wengi kubaki kua tegemezi wa ajira hivyo na kukosa ajira kabisa, zaidi ya hapo serikali inaweza kuchukua hatua stahiki ili kutokomeza tatizo la ukosefu wa ajira kama vile.
•Serikali inapaswa kupitia upya mtahala wao ili kuboresha mfumo wa elimu pia inatakiwa kupitia mfumo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Hapa mwanafunzi hata yule mwenye kiu ya kusoma ufundi apate mkopo kama au zaidi ya yule ambaye anasoma taaluma tofauti kama ualimu.
Kuwepo kwa mashindano ya kusaka vipaji na kuwaendeleza
Hapa kuna vijana wanaweza kujikita katika fani ambayo itaweza kuwasaidia wao kwenye soko la ushindani zaidi ya kukaa nyumbani na kusubiri ajira au kutembea na bahasha mikononi.
Serikali kuboresha ada zao kua nafuu.
Hapa serikali inatakiwa kufanya ada kua nafuu na kua rahisi kwa vijana kuweza kusoma fani wanazo penda. Mda mwingine mwanafunzi ilamulazimu kwenda kusoma fani ambayo pengine si rafiki kwake kwa sababu ya ada kua kubwa kwa fani anayoipenda.
Kwa mfano hapa Tanzania ada ya ualimu inaonekana kua ndogo zaidi ya ada ya mwanafunzi anaye soma Biashara au Sayansi ya technologia na mawasiliano. Hivyo kwenye kozi kama technologia ya mawasiliano ambayo mwanafunzi anaweza kujiajiri kunakuwapo na ada kubwa hivyo mwanafunzi kushindwa kuimudu na kumubidi akimbilie palipo na uahuweni wa ada hivyo anakupamba na ukosefu wa ajira.
Mfumo wa elimu upitiwe upya
Hapa serikali ifanye maboresho kwenye mfumo wa elimu yetu yaani hata uchaguzi wa wanafunzi kwenda vyuoni umushirikishe mwanafunzi mwenyewe. Kwa Tanzania inaonekana kutojali kipi mwanafunzi anapenda kwenda kusomea licha ya kuwepo na fomu za kujaza nini mwanafunzi angependa kusomea lakini hilo ni kama halifuatwi na kua kama lipo kama ubabaishaji.
Kwa mfano mwanafunzi anaweza kuchagua kusomea Udaktari, uhasibu, uhandisi, ualimu na ugavi, lakini uchaguzi ukija mwanafunzi huyo anajikuta amechaguliwa kwenda kusomea Ukutubi licha ya mwanafunzi kua na vigezo vya kusomea kozi Alizo omba. Hivyo serikali iliangalie hili.
Endapo serikali ikiyapitia haya elimu ya Tanzania inaweza kua bora na kuondoa nadharia ya vijana kua Elimu ya sasa ni kama kubeti kwa sababu wapo wengi wamesoma na hawana ajira na kuonekana si bora hata zaidi ya vijana ambao hawajakanyaga shule.

Upvote
48