Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari,
Kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana huamua kuhamia mijini kujaribu kutatua changamoto hizo.
Lakini pamoja na wimbi hili la vijana ambao ni nguvu kazi kuhamia mijini lakini bado jamii zinaendelea kukumbwa na changamoto zaidi.
Umaskini, ujinga(kukosa elimu), na maradhi bado ni mtego kwa mamilioni ya Watanzania.
SERIKALI NA JAMII KWA UJUMLA IFANYE MAMBO TAFUATAYO KUPUNGUZA WIMBI LA VIJANA KUHAMA VIJIJINI NA KUHAMIA MIJINI ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI NA VIJANA KWA UJUMLA.
1. Kuanzisha miradi ya kikanda.
Hapa serikali inapaswa kuanzisha miradi mikubwa kikanda kulingana na uoto wa sehemu husika au kulingana na shughuli kuu za sehemu husika.
Mfano
1: Serikali itatakiwa kuanzisha mashamba makubwa ya mikorosho mikoa ya Lindi na Mtwara, vijana wataingizwa kwenye miradi kama sehemu ya wamiliki washiriki (wanahisa) kwakuwa ndio watakuwa nguvu kazi. Serikali itawajibika kutafuta wataalamu, kuwekeza vifaa vya kisasa vya kazi na kufadhili mradi kwa ujumla.
Mfano
2: Serikali itatakiwa kuanzisha vitalu vya uvuvi ziwa Victoria, ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa. Hapa serikali itawajibika kutafuta wataalamu na kufadhili mradi.
Sehemu ya mavuno itakapouzwa serikali itapata fedha na vijana watapata fedha pia. Hivyo fursa zitakuwa zimewafuata vijana waliko huko vijijini hali itakayopelekea kupungua kasi ya vijana kuhama vijijini kuhamia mijini (Rural to urban migration).
2. Kujenga vyuo vya ufundi kila kata na kufadhili masomo ya muda mfupi kwa vijana wa maeneo husika.
Kama serikali ilivyoweza kujenga sekondari kila kata vivyo hivyo serikali inapaswa kujenga vyuo vya ufundi kila kata ili kuwapa ujuzi na stadi za maisha vijana waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne lakini wamekosa fursa zingine za kielimu na kibiashara.
3. Kutoa mikopo rahisi ya vitendea kazi kwa vijana wenye taaluma ya ufundi.
Wapo vijana wenye ufundi ama ujuzi walioupata VETA na vyuo vingine vya ufunfi, na wengine wamepata ujuzi mitaani. Hawa wakipatiwa mikopo rahisi ya vitendea kazi kama granding machine, air compressor n.k wanaweza kuanzisha viwanda vidogovidogo mahali waliko na wasione tena haja ya kwenda mijini huku wasijue wanakwenda kufanya nini hukojini. Hivyo jamii itaneemeka na umaskini utaondoka kabisa. Hapatakuwa na haja tena kwa vijana kwenda mijini kutafuta ajira au kufanya ujasiriamali ambao hauna tija kubwa kwa taifa(ujasiriamali wa kuuza bidhaa kutoka nje ya nchi).
Asanteni.

Upvote
1