Serikali inayowaza kumnyonya Mtanzania kwa tozo haitawaza kupunguza kodi kwenye bidhaa ili kupunguza mfumuko wa bei

Serikali inayowaza kumnyonya Mtanzania kwa tozo haitawaza kupunguza kodi kwenye bidhaa ili kupunguza mfumuko wa bei

Natakakutulia

Member
Joined
Jan 20, 2020
Posts
59
Reaction score
390
Serikali ya CCM inayoongozwa na Raisi Samia haiwezi kufikiria cha kufanya angalau kupunguza uchungu anaopitia mwananchi kwa sasa wa kupanda kwa bidhaa karibu zote nchini.

Serikali hii inachowaza ni kupata pesa ili wao waendelee kunufaika ndii maana wamelundika tozo na kodi za kila aina, zingine hadi unazilipa mara mbili au 3 zikiwa na majina tofauti, yaani tozo kodi na ushuru kwenye kitu kimoja.

Ingekuwa wanaguswq nq mqisha ya mtanzania wangeondoa tozo kwenye miamala, wqngeshusha kodi kwenye bidhaa muhimu, wangeondoa tozo ya takataka mpaka uchumi wa dunia ukae sawa ili angalau mtanzania aweze kumudu maisha.

Lakini leo unamwambia Mfanyabiashara ashushe bei huku wewe hushushi kodi inawezekana? Na wakati huohuo Rais alishawaambia kuwa bei zitapanda na kupanda hivyo wanapandisha maana tayari walishapewa kibali cha kupandisha.

Maisha yamekuwa magumu sana na wao hawaoni uchungu maana walipwa posho na kununuliwa kila kitu hivyo hawajui mtu unavyoumia kuoandishiwa au kuingezewa gharama yoyite kwenye maisha.
 
Tunanyonywa! Sisi wadhambi msamiati kama huu hutupa tabu sana..🤣

Tukichoka tutawatoa tu hakuna namna
 
So tulikubaliana tuchague CCM,maana CHADEMA walituchelewesha sana kupata maendeleo,au mmesahau?
 
👏👏👏👇
7UID.jpeg
🐒🐒🐒👇
022040141919.jpg
 
Serikali ya CCM inayoongozwa na Raisi Samia haiwezi kufikiria cha kufanya angalau kupunguza uchungu anaopitia mwananchi kwa sasa wa kupanda kwa bidhaa karibu zote nchini...

Wako hapo juu ya meza:

IMG_20220405_112819_728.jpg
 
Wananchi wamefichwa chini ya meza wasione wanavyo sosomola.

Meza imebebeshwa hao walioko huko chini. Ujasiri wa kuondoka tu hapo chini kungeimaliza karamu hiyo.
 
Kama huwezi kuendana na beats ya mama samia hama nchi .....watu wa kulalamika kila muda ni watu wa kupuuzia
 
Back
Top Bottom