Serikali ingefanya yafuatayo ili kilimo kiwe ajira

Serikali ingefanya yafuatayo ili kilimo kiwe ajira

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Miaka kama minne hivi nilikutana na bro mmoja anafanya kazi shamba la mzungu, alikuwa ameacha kulima viazi.

Nikamuuliza kwanini, akasema kulima ni ujinga, akaniambia kuwa gunia la viazi ni 18,000 wakati kipindi wanunuzi kutoka Zambia, Malawi na Congo wanakuja gunia ilikuwa 30,000, serikali ikafunga mipaka.

Bosi wangu mmoja alilima ekari 30 za mahindi, bei ikaporomoka hajalima tena. Watu wenye mitaji mikubwa hawawezi lima kama hamna faida.

Miaka ya 60 China walikuwa na sera kama zetu, ilikuwa ukilima nafaka unatakiwa kuiuzia serikali kwa bei iliyopangwa, ya chini.

Miaka hiyo kulikuwa na njaa kali na mamilioni walikufa. Wakaja na solution, wakaita Family grain responsibility, kwamba serikali inanunua gunia kadhaa kutoka kwako na zinazobaki unaweza kuuza popote kwa bei yoyote utakayopata.

Matokeo ni kuwa uzalishaji wa kilimo ulianza kukua kwa 10% kwa mwaka. Kilimo chetu hakikui, ni cha jembe la mkono na vijana wanakikimbia sababu hakina faida.

Hata ulete mbolea na matrekta lakini kama mtu hapati faida kwenye kilimo ni kazi bure.

Serikali ifanye nini? Iruhusu watu watafute masoko mazuri popote watakapoyapata na yenyewe ndiyo iwe na jukumu la kuweka chakula cha dharura.

Na hii isiwe kuwa mwaka huu wanafungua mpaka mwaka huu wanafunga au wanafungua kisha wanaweka kodi kubwa, mtu anatakiwa anapoanza kulima anajua bei na soko lake.

Kilimo kikiwa na faida, vijana wataenda kulima, watu watanunua matrekta, mbolea, pump za kumwagilia na benki zitawakopesha.

Leo tunazalisha tani 16m za nafaka huku mahitaji ni 13m, tuko kwenye hatari ya njaa muda wote maana hata hiyo 16m haiaminiki.

Mwandishi mmoja aliandika hivi kuhusu serikali kufunga mipaka, alisema kuwa watu ambao huangusha nchi ni watu kutoka miji mikubwa, alisema, sababu kubwa ya watu kuandamana na kuangusha nchi ni kupanda kwa bei ya chakula.

Hivyo serikali hufunga mipaka ili watu wa mijini wapate chakula kwa bei ya chini huku wengi vijijini wakizidi kuzama kwenye umaskini. Bahati mbaya hii mbinu hupunguza uzalishaji na kuongeza hatari ya njaa.

Napendekeza tuanze ni EAC, mtu wa Ruvuma auze mahindi yake Juba au Nairobi kama anavyoenda kuuza Dar au Mwanza.

Nchi yetu inaweza lisha EAC yote, tutumie hiyo fursa, South Sudan wana eneo la kilimo zuri na kubwa pengine kuliko hata letu, siku wakiacha ngumi tutajutia hii fursa.

cc Rebeca 83 Malcom Lumumba Chige
 
Utaambiwa umetumwa na mabeberu,haiwezekani wapiga kura wangu wafe na njaa
 
What an article , be blessed, but here is the problem, ccm has no such brains, they dont see or think beyond buying opposition figures, stop free speech and killing where they like, this our land will remain very very poor coz of a serikali that knows nothing abaut policy implimenting and seeing them thro, again asante sana
 
Wananchi wana haki ya kuuza mazao yao ila pia Serikali inawajibu wa kusimamia hilo haswa pale chakula kinapouzwa nje ya nchi
 
Umeandika vizuri sana, nasubiri mtaalamu Chige ashushe vitu hapa, maana yeye ana ufahamu sana na haya mambo. Lakini ntarudi mkuu.
 
Nikweli kabisa.
Vijana wengi wamjini tunaomitaji yakutosha kuwekeza kwenye kilimo lakini shida kubwa iko kwenye hio mifumo yakilimo iliopo nchini.
Hakuna data sahihi zinazohusu kilimo kupelekea iwe ngumu mtu kuamua alime nin, support ya serikali na taasis za kifedha nindogo mno, soko pamoja nasystem yote inayotumika kufikisha mazao kwa mtumia wa mwisho ni mbovu imejaa udalali kwenye kila hatua.
Kilimo ingekua nifursa kubwa kwa vijana nchini sababu haichagui mwenye vyeti au asio navyeti tatizo nikama imepuuza au inachukuliwa poapoa
 
Acha tuzibiane fursa huku Kenya wakitupiga vikumbo na tunabaki na kilimo kwanza kwenye ilani zetu
 
Back
Top Bottom