Serikali iongeze marupurupu kwa mwalimu

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Marupurupu ni motisha kubwa ya kazi katika sekta zote na ni muhimu ili kuamsha ali ya wafanya kazi. Hivyo napendekeza serikali kuweka marupurupu (per diem) kwa mwalimu katika matukio yafuatayo;

Kuandaa mitihani ya ndani na nje, hapa ni pamoja na kuandaa mitihani ya mid-term na annual examination ambayo ndio mitihani inayojumuisha na likizo za wanafunzi. Pia mitihani ya mock mkoa na wilaya mwalimu alipwe per diem ili kumuwezesha kutunga mitihani bila stress

Kusahihisha mitihani ya ndani, kama wafanyavyo kwa mitihani ya necta wafanye na mitihani ya ndani kama vile mid term na annual examination

Zamu za walimu, hapa mwalimu wa zamu anahitajika kupata per diem katika wiki yake ya kudamka kila siku kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika nidhamu, usafi na masuala mengine ya kiusalama na kiafya

School tour, kuna zile ziara au study tour hapa mwalimu apewe per diem kwa kazi ya kuwapeleka wanafunzi na kuwarudisha wakiwa salama na wakiwa wamepata elimu ya mazingira

Note: kuwepo kwa hayo marupurupu kutapunguza njaa za kugombania kusimamia uchaguzi
 
pia kiwango cha chini kwa walimu kiwe degree kwa ngazi zote
 
We mwalimu kwa akili gani uliyonayo unataka upewe hela? kwa kipi unachofundisha? Division one zinatoka hazijui hata kujielezea! Kw3nda huko mwizi wewe!
Unavyojiona wewe una akili hizo akili amekupa mwalimu acha dharau
 
Ndio lakini wanaosimamia ni walimu pamoja na kupokea mwenge 😄 🤣
Hiyo yote ni kwakuwa hawapewi marupurupu kwenye idara zao wakipewa huko hawaendi kuvamia kazi za watu wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…