gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 790
- 1,373
Kutokana na uendeshaji wa shirika la DART kusuasua, na kwamba zaidi ya magari 70 kufikia kuwekwa pembeni kutokana na ubovu na madereva kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutokutoa huduma zinazo ridhisha, ni wakati sasa kwa serikali kuongeza mwekezaji mwengine kwenye njia hiyo ili kukuza ushindani.
Pamoja na hayo, barabara ya Mbagala tangu izinduliwe haikuwahi tena kufanya kazi ya kupitisha mabasi ya mwendokasi jambo ambalo lingepunguza adha ya usafiri kwa abiria, ili kuifanya DART kufanya kazi kwa ufanisi, ninapendekeza ziongezwe kampuni mbili zaidi kila mmoja iwe na mabasi yake na zote zipewe haki ya kutumia barabara ya mwendo kasi.
Serikali iwekeze kwenye usimamizi na kukusanya mapato yake.