mwanyika Jr
New Member
- Jun 6, 2024
- 1
- 0
Serikali itengeneze mpango maalumu wa namna ya kupanga miji na vijiji ili kupunguza gharama za kuhudumia miundombinu yake. Hii inamaana kwamba ili kifikia lenho lazima tuwe na mwendelezo sahihi wa ujenzi wa nyumba, viwanda au maendelezo yoyote yale ya ardhi.
Miji mingi inamaeneo ambayo ni wazi au chakavu kabisa na wanilik wa maeneo hayo hawaweza kuyajenga na hawajauzi kwa kigezo cha kwamba yaongezeke dhamani. Hali hii hufanya mji kutokuwa na mwonekena mzuri na kufanya watu wenye utayari wa kukuza mji kwenda kujenga pembeni mwa mji ambako kunapatikana maeneo ya kuuzwa.
Hali hii itaichangia serikali kuanza kufikiri namna ya kupeleka miundo mbinu nje ya mji bila ulazima kama maji, barabara, umeme na vinginevyo.
Mfano. Unakuta mtu amejenga nyumba km 20 kutoka mjini baadae wanaongezeka wanakuwa watu hata 100 wanaanza kudai shule, hospitali na mengineyo wakati meneo meng mjini yapo wazi wangejenga hapo ambapo huduma zote zipo.
Pili, gharama kubwa za kuuboresha miundo mbinu. Mfano kunakijiji kipo wilaya ya makete umbali wa kilomita zaidi ya 60 kutoka ikonda hospitali kilihitaji umeme wa rea na kimepelekewa. Idadi ya nyumba hazifiki hata 100. Hapa katikati hapan makazi ni maeneo tu yanamilikiwa na watu na hawataki kuyatoa. Hiyo serikali imetumia gharam kubwa kuwafikishia umeme zaidi ya gharama ya kuwalipa fidia wananchi warudi kujenga karibu na ilipo Miundombinu yote.
Serikali iweke mpango sahihi wa unilikishaji na uendelezaji wa Ardhi. Mfano kama serikali ikipima viwanja 1000 mtu ambaye anaanza ujenzi kwa wakat huo apewe kiwanja kwa bei nafuu aili aweze kujenga, kisha atakaye fuata kujenga auziwe kinachofuata mbele yake. Hii itasadia kujua kwamba mwaka huu tumetoa vibali kadhaa vya ujenzi na jyumba zimesogea kwa kilomita nne. Hivyo barabara itaongezwa umbali huo. Sio kutengeneza kilomita 40 kumfuata mtu mmoja au 10.
Serikali isiuze viwanja kiholela mtu ananunua viwanja 30 kwa bei ndogo anaacha kuendeleza ili aje auze kwa bei kubwa zaidi, hii inafanya mji kukua taratibu hasa maafisa wa Aridhi. Pia inafanya ujenzi holela na watu kujenga sehemu zisizo na miundominu mizuri.
Umilikishaji wa Ardhi bila kutaja muda wa Uendelezaji unailetea serikali gharama na mzigo mkubwa katika kuhudumia wananchi, lakini pia inazalisha migogoro mingi ya Ardhi kwa wananchi na serikali yake.

Upvote
2