Serikali ipige marufuku viwatilifu vyenye "Atrazine"

Serikali ipige marufuku viwatilifu vyenye "Atrazine"

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Wanajamii mambo sio mambo, leo nitawapasha habari juu ya sumu ya kuulia magugu Atrazine.

Hii sumu inatumiwa sana na wakulima katika kuua magugu katika mashamba makubwa ya mazao mbalimbali: miwa, mahindi. Sasa kwa nini hii sumu ni Nongwa?

Mwaka 2010, Dr. Tyrone Hayes alifanya utafiti kwa Vyura waliokuwa wana ishi ndani ya maji yenye hii sumu kwa kiwango kidogo kinachoruhusiwa na mamlaka za maji safi huko nchini Marekani, na kubaini ya kwamba vyura wa kiume walibadilishwa jinsia na kuwa wa kike.

Swali linakuja uwepo wa hii sumu kwenye vyakula vyetu itafanya watoto wetu wa kiume wawe wa namna gani?

hapa chini nitaambatanisha picha mbili, moja ni ya chura wa kiume ayebadili jinsia akiwa kakamatiwa akitagishwa mayayi. Na picha ya pili huu ni ukurasa kutoka "registered pesticide to use in united republic of Tanzania" toleo la feb 2020, kwenye hiyo list iyo sumu inapatikana kwenye page nyingi sana.

Hivyo basi ndio maana nipo hapa nikilia na Serikali yangu ijaribu kwa namna yakee kuzuia mafuriko ingawa imechelewa kidogo.

Gay-Frogs.jpg
Screenshot_20220702-090708.png
 
Duh naona pia imekuwa manufactured South Africa.

Hao makaburu mara zote wamekuwa na agenda mbaya juu ya race yetu.
 
Jana nilikuwa sabasaba nao pia huwapa samaki dawa kuwabadili jinsia sijui tunaokula hao samaki tunaepukaje hayo madhara
 
Duh naona pia imekuwa manufactured South Africa.

Hao makaburu mara zote wamekuwa na agenda mbaya juu ya race yetu.
Huwa hamkosi wa kumlaumu,vipi ile "vita ya uchumi" na Makinikia mliokuwa mnaikatia viuno mkawa mnamlaumu Tundu Lissu?
 
Huwa hamkosi wa kumlaumu,vipi ile "vita ya uchumi" na Makinikia mliokuwa mnaikatia viuno mkawa mnamlaumu Tundu Lissu?
Bado inaendelea.

Juzi hapo Spika kwenye ishu ya Ngorongoro alisema tupo kwenye vita vya kiuchumi.
 
So hawa mashoga hapa sinza wametokana na hizo viwatilifu

USSR
Mapunga ya tz yote yakiulizwa yanasema yana matatizo ya homoni na kujikuta yako hivyo..ila waarabu walituharibia sana jamii zetu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom