Serikali ipo kuimarisha misingi ya elimu au kuiteketeza ?

Happycuit

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2013
Posts
646
Reaction score
542
Jamani wakubwa humu,habarini zenu,,,


awali ya yote naomba kujua NACTE ni chombo cha serikali au binafsi? maana naona kuna mchezo mchafu wa watu wachache umeandaliwa ili kujitengenezea mazingira ya kipigaji kwani ktk hivi vyuo vya ualimu vilivyohamishiwa kutoka WIZARA YA ELIMU KWENDA NACTE wakuu wamepata sababu za kudanganya wanachuo kila wanapodai mahitaji yao ya msingi kwa kusema kuwa lengo la serikali

kuhamisha jukumu la kusimamia vyuo hivi ni kujitoa moja kwa moja ktk kuvihudumia ikiwemo kutovitumia ruzuku,hivyo hivi vyuo vinajitegemea vyenyewe na ndio maana ada imeongezwa maradufu kutoka laki 2 ya awali mpaka laki 6...pamoja na michango yote inafikia laki8.5


kwa ilivyo kawaida kada ya ualimu ni ya watu wa kati kama sio wa chini je,wataweza kumudu hizi gharama kwa miaka 3?au wenzetu mlifikiria nini?

tujadili wadau
 
Michango ni mingi isiyo na tija,ukihoji unaambiwa kama umeshindwa beba begi lako rudi kwenu....nanukuu jibu la mkufunzi "walimu hatulipwi kwa wingi wenu hapa, nikifundisha watu 100 na nikifundisha watu 8 mshahara ni uleule, kama wewe umefuata ualimu soma chukua nenda ila kma umefata kudai haki ondokaaaa"

dah.. nilitamani nimchape kofi
 
toka siku ya kuripoti tar6/10/2014 mpaka leo haijawahi kupikwa chakula kingine zaidi ya ugali na maharage na asubuhi chai tupu,

huku ukiumwa unaweza kufa unajiona hakuna huduma za kuridhisha za afya,licha ya kuchangia pesa za huduma ya afya pamoja na zile za tahadhari.


pesa za serikali ya wanafunzi na zile za michezo ni mradi wa wa hawa wachumia matumbo.


pesa za ukarabati wa miundombinu ndio dah!


tunasoma tehama ila toka semista ianze mpka leo tunaelekea mwisho wa semista hakuna kompyuta hata moja inayofanya kazi licha ya kulipishwa pesa za ukarabati wa miundombinu ya kompyuta.

kuna walimu toka chuo kifunguliwe hawajawah kanyaga clas ila mitihani inakuja tu.

ukihoji unajibiwa maneno ya khanga
 
Last edited by a moderator:
Happycuit


NACTE ni chombo cha serikali na kipo chini ya wizara ya elimu,sema demand ya walimu imeanza kupungua.KWA KIASI KIKUBWA WANAFUNZI WALIOENDA FANI YA UALIMU NI TABAKA LA CHINI NA HIYO ILIWAFANYA WADUMU MUDA MREFU KWENYE HYO KADA LAKINI WAKIANZA KWENDA TABAKA LA KATI NA JUU, TURNOVER YA WALIMU ITAKUWA JUU.HAWA WANAKUWA WANATAFUTA NJIA YA KUTOKEA TU.
 
Last edited by a moderator:

ahsante mkuu kwa mchango wako,ingawa bado nina swali kichwani mwangu la kuwa ni kweli kwamba serikali imeacha kuvihudumia hivi vyuo au ni propaganda tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…