Serikali ishukuru Mashabiki wa Simba wamevunja viti kuliko wangeamua kumshughulikia mwamuzi

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,271
Reaction score
2,903
Kwanza niseme wazi wazi kabisa huwa sikubaliana na njia za matumizi ya nguvu kwenye maamuzi yoyote yale. Lakini pia wanasema binadamu ukimnyima haki yake mwishowe huamua kuchukua kwa nguvu. Na tuliona huko South Afrika kipindi cha ubaguzi, Msumbiji, Angola n.k lakini sipendelei sana maamuzi ya namna hiyo.

Serikali ishukuru kuwa wanachama wa Simba waliamua kuvunja tu viti, wasiwasi wangu ilikuwa kama wangeamua kuingia ndani ya kiwanjani kuwashughulikia waamuzi nadhani hali ingekuwa mbaya zaidi. Hapo kusingekuwa na malipo ya kutosha ya uhai au viungo vya waamuzi hao.

Hivi ni wangapi wakikasirika hupiga meza? Namfahamu mheshimiwa mmoja ni mtu mkubwa sana, sana kwenye serikali. Alikasirika siku hiyo ofisini kwake akapiga meza ngumi na kusukuma kompyuta iliyokuwa mezani ikaanguka. Waliokuwa pamoja naye waliogopa sana lakini walimsifia kuwa anachukia sana uonevu baada ya kusikia kuwa kuna maskini wameonewa sehemu flani. Niliambiwa aliletewa kompyuta nyingine kesho yake bora kuliko ile ya kwanza.

Nilipomwambia jambo hili mwalimu wangu ambaye ni Dr pia wa saikolojia akanambia ni afadhali alipiga ngumi meza maana angekuwa hajajua namna ya kuhamishia hasira yake basi angepiga mtu na pengine angeua mtu.

Ni wangapi wanaudhiwa ofisini na boss wanakuja kushusha hasira zao kwa paka au mbwa analewalilia miguuni wakiwa nyumbani? Serikali ijitahidi kuwaambia TFF waelewe umuhimu wa michezo na maana yake kwa wanagenzi. Maana kama tusipokuwa makini tukumbuke habari za Escobar aliyekuwa mchezaji wa Colombia baada ya kufungisha goli aliuawa na mtu mwenye hasira kali. Kumbe mtu huyu angepata nafasi akang'oa kiti kimoja au viwili hasira zake zingeisha.

Lakini nasisitiza mashabiki wa team zote tusifanye fujo za namna hii. Wakati mwingine ni bora kushughulika na anayesababisha tatizo kama hilo na si vitu.

List ya matukio ya vurugu uwanjani hapa duniani. List of violent spectator incidents in sports - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Busara zaidi inahitajika kwa waamuzi wanaochezesha mapambano makubwa ktk michezo ya aina zote.
 
Mbona nyinyi watu wa Matopeni mnatapatapa sana kila dakika mnaanzisha uzi mpya kuongelea swala lile lile? Jana Arsenal kashinda goal la mkono but hatujaona kiti hata kimoja kiking'olewa.
 
If the facts are on your side, pound the facts into
the table. If the law is on your side,
pound the law into the table. If
neither the facts nor the law are on
your side, pound the table.
 
Hasira zingine za kijinga tu hakuna kupiga ngumi wapi wala wapi. kama kweli mtu anahasira ajikung'ute mwenyewe tuone!!!!
 
Utakuta mtu ni mshabiki wa arsenal na pia yupo simba lakini mtu huyohuyo analisifia goal la arsenal lakin kwa upande wa simba analalamika,hapa ndo ujue kwanini hawa ni mbumbumbu.
 
Utakuta mtu ni mshabiki wa arsenal na pia yupo simba lakini mtu huyohuyo analisifia goal la arsenal lakin kwa upande wa simba analalamika,hapa ndo ujue kwanini hawa ni mbumbumbu.
We si useme wazi kwanini mbowe anashangilia goli LA tambwe wskati huohuo anampinga Jecha
 
huu ni mpira na ni michezo hizo chuki zipeleke kwingine.
tumeshuhudia makosa mengi katika soka lakini yanaishia uwanjani.
kama vita nendeni congo mkapigane
 
Kwanza mshukulu mmepata angalau sare.
Acheni kulialia jipangeni upya.
Maradona alitwaa kombe la dunia kwa goli la mkono na haukufutwa na watu hawakung'oa viti.
Kama fungeni na nyinyi goli la mkono lefa akilikubali mnapeleka kati.
Mnalialia tu kama watu wasiojua sheria za soka bwana.
Refalii ni binadamu kama nyinyi, kafanya makosa kama mliofanya nyinyi ya kuvunja viti.
 
Pametokea taharuki kanisan baada ya paroko kusema tuwapongeze Yanga kwa goli la *Tambwe*[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


Hivi nnavyoongea viti vyote kanisan vimeng'olewa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapa habari sio goli hapa ni mtiririko wa matukio ya mashaka dhidi ya upande mmoja ndio yaliyoamsha ile hali.
 
Achen kutetea ujinga,serikali haihitaj kushukuru bali juwashugulikia wale walioonekana kwenye pcha wakivunja viti baas, maana hzo habar zbatokea tz tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…