A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mkazi wa Kibaha kwa Mfipa, Kata ya Viziwa Ziwa, Kitongoji cha Sagale Kabimbini (Sauti ya Umma) Mkoani Pwani.
Ninajitokeza kuandika malalamiko kwa niaba ya Wananchi wenzangu zaidi ya 340 tunaoishi katika eneo hilo nililolitaja juu.
Tunaamini kupitia JamiiForums ujumbe huu utafika katika mamlaka husika na hatua zitachukuliwa na tutapata msaada unaotakiwa hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya tunaolalamika ni Wananchi wa kipato cha chini ambao wengi wetu hatujui masuala ya Kisheria au taratibu za masuala ya ardhi.
Hivyo, kuna watu wanataka kutumia nafasi hiyo kutuonea na kuchukua kile ambacho tunastahili kuwa nacho.
MGOGORO WA ARDHI KIBAHA KWA MFIPA, KATA YA VIZIWA ZIWA, SAGALE
Kwa zaidi ya miaka nane sasa, kumekuwa na watu wanaojiita NIKO, MAJEJE, na NAFTAL wamekuwa wakitusumbua na kutunyanyasa Wananchi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Kibaha kwa Mfipa.
Wanatengeneza ramani za kughushi na kwa kuwa Wananchi hatuna uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya ardhi, wanataka kutufukuza na kuvunja nyumba zetu huku wakiwa hawana umiliki halali.
Zaidi ya Wananchi 340 na makazi zaidi ya 220 yapo hatarini kuharibiwa kutokana na watu hao kutumia ujanja-ujanja kutaka kutuumiza Wananchi.
Kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Kibaha alifika eneo hilo, lakini alionekana kutojali nani mwenye umiliki halali kati ya wale wanaojiita wawekezaji na Wananchi.
Tulitegemea DC anapofika kwetu awe na majibu kuwa eneo hilo linamilikiwa nan ani kihalali na kama ni Watu hao kweli miaka yote waliku wapi mpaka Wananchi wamuziana na kupita vizazi kadhaa bila wao kujitokeza.
DC hakuna majibu hayo, badala yake alifika na kuuliza tu nani anataka kuingia makubaliano ya kuuziwa kihalali? Yaani Wananchi tununue maeneo yetu kwa mara ya pili la sivyo wanataka kuvunja.
Kinachotupa mashaka ni mambo mawili, kwanza DED naye alituita baadhi ya Wananchi na kusema wahusika hao wapo tayari kuuza eneo hilo kwa Tsh. 7000 kwa ‘Swea Mita’ lakini kasema “Sio mtoke hapa mkatafute Wanasheria wenu wa Mtaani.”
Tunachojiuliza kama suala hilo ni la halali, inakuwaje Kiongozi kama huo anataka tusishirikishe Wanasheria, wao si wanataka kuuza kihalali? Hapo kuna kitu hakipo sawa.
Pili kuna wakati tulifuatilia Wizara ya Ardhi kuulizia maeneo tunayokaa kwa kuwapa locationa kamili wakasema maeneo hayo hayapimwa na hayana mmiliki aliyejiandikisha Serikali, sasa kama ni hivyo hao watu watatu wanatoka wapi?
Watu hao ambao tukiwauliza nyaraka zao za umiliki hawaoneshi zaidi ya kuonesha ramani ambayo mtu yeyote anaweza kuwa nayo, pia walikuwa na kesi za masuala ya ummiliki Arusha na Mwanza, hali inayoonesha wanashirikiana na baadhi ya Watu Serikali katika michezo yao.
Ujumbe huu ufike kwa Waziri wa Ardhi, Waziri Mkuu na Rais Samia wajue kuwa Wananchi wao huku tunateseka na tupo mbioni kubomolewa nyumba na hao watu ambao inawezekana ni matapeli wanaoshiriana na baadhi ya watu wenye nafasi Serikalini.