Serikali isipochukua hatua kali kwa Wafanyakazi wa TRA wanaotuhumiwa kwa rushwa, wafanyabiashara wataathirika milele

Serikali isipochukua hatua kali kwa Wafanyakazi wa TRA wanaotuhumiwa kwa rushwa, wafanyabiashara wataathirika milele

Magufuli 05

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2023
Posts
1,433
Reaction score
2,791
Hima hima Tanzania.🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Waziri mkuu, Jana tarehe 17/05/2023 katika mkutano wako na wafanyabiashara wa k/koo asilimia kubwa ya wachangiaji waliwanyooshea kidole baadhi ya wafanya kazi wa TRA kwa RUSHWA iliyokithiri.

Kilichonishangaza hukutoa Kauli yoyote Kali ya kushughulikia changamoto hiyo zaidi ya kusema TRA badilikeni na mjitathmini.

Serious?

Yaani mpiga dili uishie kumwambia mjitathmini tu? Nani mjinga wa kuambiwa badilikeni na akabadilika kirahisi hivyo?

Mimi nionavyo serikali ya Rais wa sita haiko makini na pengine inadhamira ndogo Sana ya kupambana na RUSHWA.

RUSHWA kwa mamlaka ya mapato haiko Kariakoo pekee ni kilio cha nchi nzima.

Hii RUSHWA munayoilea ndiyo imewakatisha tamaa watu wengi wakiwemo wafanyabiashara kulipa Kodi wakiona inanufaisha kikundi cha watu.

Kamati ipi uliyounda ikaleta tija kwa nchi, Ile ya kuungua kwa soko la k/koo mpaka leo haijawahi kuleta majibu, leo unaunda kamati nyingine tena?

Pole Tanzania🇹🇿
 
Back
Top Bottom