Serikali isiyohitaji kodi haramu inaposhangilia mapato haramu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mamlaka za serikali zimekuwa kero kubwa kwa wananchi. Uliza across the board labda kama wewe ni mlamba asali au familia zao.

Kuna hoi hoi na nderemo kuwa zakusanywa 2Tn/- Kwa mwezi. Humo zimo tozo batili zinazoambana na tozo za Mwigulu, faini za yanayoitwa makosa mbalimbali hata ambayo ni batili. Malipo kama haya yapo mengi.

Kwanini kuwapo tozo zozote za ziada kwenye miamala ya kulipia malipo ya serikali. Kwanini wananchi kutozwa faini kwa sababu ya mapungufu yoyote yatokanayo na utendaji wa serikali yenyewe au mifumo yake?

Ole wako deadline ya malipo ipite. Kuelekea deadline utasikia "mtandao unasumbua."

Kukithiri kwa faini batili. Angalia faini za maegesho na uhalali wake.

"Si nadra kuona mabasi yakitozwa faini za maegesho hata sehemu zenye vibao vya Tanroads vyenye kuruhusu mabasi kuegeshwa sehemu husika."

Imekuwa vurugu mechi. Kinachotakiwa ni mapato bila kujali uhalali wake.

Si kuwa watu wanalipa faini nyingi hizi shingo upande kama yalivyomkuta Simba wa Tandale? Si kuwa Simba ana hoja ila katereza tu kwenye kuiwasilisha?

Vipi Kodi za kubambikizwa, vipi mapato ya kulazimishwa kununua mashine za EFD, ving'amuzi vya magari nk? Izingatiwe vingi vya hizi vinauzwa kwetu ya x 100 kulinganishwa na China huko vinakozalishwa?

Vipi utitiri wa kodi kwenye bidhaa au huduma moja? Kwani ni nadra kukuta bidhaa ikiwa na kodi zaidi 100%? Agiza kitu kutoka nje ujute!

Malipo haramu kwa serikali ni aibu labda kwa wahuni.

Tuzingatie wahuni si watu wazuri!
 
Dalili za kuchoka akili za wanaotuongoza, hawana muda tena wa kujiuliza hiki kimetoka wapi kwa njia gani, wao ilimradi wamekusanya mwisho wa siku zihesabiwe tuambiwe zimepatika 2tn tuwashangilie, naona hata nasi tumechoka akili pia, viongozi wanajiendea tu, na tunaoongozwa tunajiendea zetu tu..

Tumekuwa taifa la wana kondoo..
 
Tuna Gas, Tanzanite, dhahabu, almasi na madini kibao bado mbuga za wanyama tuna bandari ila Tanzania bado maskini.

Kagame alisema tumpe bandari kama sisi imetushinda.
 
Dalili za kuchoka akili za wanaotuongoza, hawana muda tena wa kujiuliza hiki kimetoka wapi kwa njia gani, wao ilimradi wamekusanya mwisho wa siku zihesabiwe tuambiwe zikepatika 2tn tuwashangilie, naona hata nasi tumechoka akili pia, viongozi wanajiendea tu, na tunaoongozwa tunajiendea zetu tu..

Tumekuwa taifa la wana kondoo..

Bila ya sisi kujiongeza na kuwakomalia watu hawa ambao wenyewe kodi haziwahusu tutegemee machungu zaidi. Jan 14 diesel juu. Wametuona mazuzu.

Ttungane kuwakataa wahuni.
 
Tuna Gas, Tanzanite, dhahabu, almasi na madini kibao bado mbuga za wanyama tuna bandari ila Tanzania bado maskini.

Kagame alisema tumpe bandari kama sisi imetushinda.

Kwa hakika wahuni si watu wazuri na hao ndiyo walioshika usukani kwa mujibu wa bwana kiroboto.
 
Jana mida kama ya saa tatu ivi na ushee usiku.....
Nienda kuonana na brother angu maeneo ya chamazi...
Opposite na uwanja wa Azam complex Kuna pub.....
Nilimkuta brother angu akiwa na rafik yake wakibadilishana mawazo huku wakipiga Moja mbili...
Nilipo fika nikawasalimia nikaketi tuka Anza piga story mbili tatu...
Gafla likaja karandinga la halmashauri ya Temeke.....wakashuka makamanda
Wakiwa na migambo wa Jiji wakaenda kukagua leseni ya biashara na vibali vingine.....
Gafla in charge aka amlisha viti na makreti ya bia yabebwe kupakizwa kwenye gari lao ...baada ya kua wameviandika Kwa markpen.....

Baada ya hapo hatukukaa sana tukaondoka....

Nilicho jiuliza nisahihi kufanyika operation kama hizo usiku....??
Ni nani ambae anabariki hilo....
Kinacho tengenezwa hapo ni dalili ya rushwa na ukandamizaji...sidhani kama utaratibu upo ivyo wa kuvizia mfanya biashara usiku.....?
 
Mondi alizingua presentation. Hoja alikuwa nayo.
 
Ungewarekodi ni wezi hao.
 
Back
Top Bottom