Pana magari almaarufu usiku kwa usiku. Haya ni haramu kwa mujibu wa sheria japo abiria wanaoyahitaji wapo, tena wengi tu.
Pana magari Hiace yanazuiliwa kusafiri umbali zaidi ya km 100. Haieleweki ni kwa mujibu wa kigezo kipi, japo abiria wenye kuyahitaji wapo na aliyeyatengeneza hana ufahamu wa mantiki ya restriction hiyo.
Pana magari Hiace, boda boda na bajaaj kuzuiliwa kuingia mijini kati kwa mujibu wa sheria, japo wenye uhitaji wake wapo.
Kuna magari mapya kwenda nchi jirani (IT) yanazuiliwa kubeba abiria kwa mujibu wa sheria, japo abiria wenye kuyahitaji wapo.
Ni mwendo wa sheria na vizingiti right, left and center kutoka serikalini.
Cha kujiuliza: ni je, kwa nini uwepo wa uhitaji wa huduma kama hizi usionekane kuwa kama fursa? Badala ya kukimbizana na watu hawa kama ilivyokuwa mapema kwa machinga, kusiwepo utaratibu mzuri wa kulipa kodi mahsusi tu?
Kuruhusu fursa kama hizi zisingekuwa na faida kama hizi?
1. Kutoa ajira.
2. Kuongeza mapato kwa serikali.
3. Kuongeza wigo wa Kodi.
4. Kuongeza wigo wa walipa Kodi.
5. Kuondoa chuki inayojipalia serikali pasipo na umuhimu.
6. Nauli za usafiri kupungua.
7. Watu kusafiri kulingana na mahitaji yao.
8. Nk, nk.
Ni mantiki ipi inayo halalisha serikali yenye kuthubutu kutamka kuwa haihusiki kuzalisha ajira kuzizuia fursa za ajira kama hizo na kwa mujibu wa sheria zake tu?
--------
Serikali isiyo na wajibu wa kutengeneza ajira ni ya nini?